Wednesday, November 4, 2015

Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt John Pombe Joseph Magufuli alimpokea Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria TB Joshua Uwanja wa ndege Dar leo jioni. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa.
TB JOSHUA (3)
Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli wakibadilishana mawazo na Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria TB Joshua mara baada ya kuwasili nchini jioni hii. TB JOSHUA (4)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi. TB JOSHUA (2)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam leo  jioni . (Picha na Freddy Maro)
  *****************
Mtume TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
 
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.
 
TB Joshua amempongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt. Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta ametangaza kuwa atawania nafasi ya Spika ili kuliongoza Bunge la 11. Sitta aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa amekuwa kada wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitosa katika mchuano wa kuwania nafasi hiyo nyeti wakati huu ambao Bunge limevitaka vyama vya siasa viwe tayari kwa ajili ya kupeleka majina ya wateule wao wa nafasi hiyo mara itakapotangazwa kuwa wazi.

Msemaji wa Spika huyo mstaafu, John Dotto alisema jana Dar es Salaam kuwa Sitta amemua kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo na uzoefu alionao wa kuendesha Bunge. Alisema Sitta anaamini kuwa uwezo wake aliouonesha katika kuendesha Bunge la Tisa akitumia kaulimbiu yake ya ‘Spika wa Kasi na Viwango’ itamfanya aendane na kasi ya utendaji wa Rais Mteule, Dk John Magufuli.

Sitta alijizolea sifa wakati akiwa Spika wa Bunge la Tisa kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, ikiwamo Bunge hilo kufanyia marekebisho ya kanuni mbalimbali zilizolifanya liwe na makali na kuibua kashfa nzito ikiwamo ya Richmond ambayo ilisababisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu na alilirejeshea makali Bunge.

Tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano limetangaza kuanza kwa mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge, atakayerithi mikoba ya Spika Anne Makinda.
 
 Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam mapema wiki hii alisema kuwa mgombea wa nafasi ya Spika, anaweza kuwa Mbunge au mwanachama yeyote wa chama kwa masharti kwamba kama si Mbunge, jina lake lazima liwasilishwe kwanza Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku tano kabla ya uchaguzi kujiridhisha kuwa mgombea huyo ana sifa za kuwa Mbunge.

Bunge hilo la Tisa lilipata ufanisi na mafanikio kadhaa kutokana na ubunifu na ujasiri wa baadhi ya wabunge wakiongozwa na utayari wa Sitta ambaye wakati akishika nafasi hiyo aliahidi kuwa ‘spika wa kasi na viwango.’

Mafanikio yaliyopatikana katika Bunge hilo ni pamoja na kutungwa kwa Kanuni mpya za Bunge za mwaka 2007, ambazo zimeelezwa kuwa zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuliwezesha lifanye kazi kwa ufanisi kama vile kuondoa ukiritimba wa serikali kuwa ndiyo pekee inayoweza kupeleka muswada bungeni.

Kanuni hizo mpya za mwaka 2007 ambazo zilitokana na kufanyia marekebisho makubwa kanuni za Bunge za mwaka 2004, zilitoa mamlaka kwa kamati za kudumu za Bunge kuwa na uwezo wa kupeleka mswada kwa ajili ya kujadiliwa bungeni na hatimaye kuwa sheria.

Msemaji  Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia.

Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.

Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.

“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,” amesema Mwambene.

Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.

“Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema Mwmbene na kuongeza.

Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.

Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeahirisha kwa mara ya pili  hafla ya vyama vya siasa kumuaga Rais Jakaya Kikwete baada ya  kumaliza miaka 10 ya uongozi wake kwa mujibu wa katiba. 
 
Hafla hiyo inayoratibiwa na Baraza la Vyama vya Siasa ilipangwa  kufanyika jana baada ya Oktoba 2, mwaka huu kuahirishwa ili kutoa  fursa kwa Rais Kikwete kushughulikia mvutano wa uchaguzi wa Zanzibar  ulioibuka kufuatia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kufuta matokeo  yote ya uchaguzi huo. 
 
Vyama vilivyoalikwa kushiriki hafla hiyo ya kumuaga Rais Kikwete ni  Chama Cha Mapinduzi (CCM), vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya  Wananchi ( Ukawa) vya Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf), NLD na vyama  vingine vya upinzani.
 
Akitangaza kuahirishwa kwa hafla hiyo  kwa mara ya pili, jijini Dar  es Salaam jana, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi,  alisema kikao hicho kimeahirishwa tena kutokana na Rais kubanwa  na  majukumu mengine ya kitaifa ikiwamo suala la Zanzibar.
 
 “Tumeamua kuahirisha  hadi siku tutakayotangaza tena kutokana na  Rais kukabiliwa na majukumu mengine na suala la Zanzibar bado  linashughulikiwa,” alisema.
 
Alisema akiwa msajili wa vyama vya siasa  amefurahishwa na hatua ya  Rais Kikwete  kulishughulikia suala la Zanzibar  kwa vitendo ili   kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa  nchini.

Friday, September 4, 2015


Pitia hapa headline mpya kwenye magazeti mbalimbali ya Udaku, Michezo na Hardnews. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MWENYEKITI Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amewataka Watanzania kumpuuza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa kwa kauli zake zilizojaa uchochezi na propaganda za siasa.

Pia alionya kauli za ovyo zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba wapinzani wakishinda vyombo vya ulinzi vitachukua nchi.

Alisema jeshi la Tanzania linasimamia misingi yake na kiongozi yeyote atakayeingia madarakani litafanya naye kazi kwa kuwa wote ni Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kufafanua mambo mbalimbali yalitamkwa  na Dk. Slaa juzi, Mbatia alisema  tuhuma alizozitoa kiongozi huyo zinalenga kuleta mpasuko katika taifa na kuvunja amani ya nchi.

Alisema hotuba nzima ya Dk. Slaa ililenga kumshambulia moja kwa moja Mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa kwa sababu amekuwa tishio kwake na kwa CCM.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema mara zote propaganda kama hizo huwa zinafanywa na chama tawala ambacho kimekwisha kuona viashiria vya kuondolewa madarakani kupitia sanduku la kura.

Mbatia alitoa mfano kuwa kitendo cha Dk. Slaa kuwasingizia baadhi ya viongozi wa dini kwamba walihongwa na Lowassa ili wamuunge mkono ni hatua ya kuwataka waumini wasiwaamini viongozi wao jambo ambalo ni hatari kwa amani ya nchi.

“Hoja alizozitoa ni nyepesi ambazo Watanzania wanatakiwa kuzipuuza na wasikubali mpasuko hasa unaoletwa kwa mlengo wa imani ya dini.

“Kuwahusisha viongozi wa dini na tuhuma za uongo ni siasa nyepesi za mtaroni.

“Kusema eti Lowassa anaungwa mkono na Walutheri kwa sababu ni wenzake ni mpasuko mkubwa katika nchi,” alisema.

Mwenyekiti huyo wa NCCR Mageuzi alisema alisikitishwa na uongo uliosemwa na Dk. Slaa kwamba hakuunga mkono kuingia kwa Lowassa Chadema kwa sababu mwanasiasa huyo alishiriki kwa ukamilifu mchakato mzima wa kumshawishi Lowassa na wenzake kujiunga na Ukawa.

“Nimesikitishwa sana na uongo uliosemwa jana na kaka yangu Dk. Slaa kwa sababu  alishiriki katika kumshawishi Lowassa na wengine kujiunga nasi katika harakati za mabadiliko ya kweli,”alisema Mbatia.

Alisema kusema kwamba Lowassa alitoa ahadi ya kujiunga na Ukawa akiwa na kundi kubwa la wana CCM ni kutunga na hauna mashiko ya katiba na kanuni kwa vile  hakuna katiba yoyote ya chama cha siasa yenye masharti kama hayo.

“Lowasa alipokuja Ukawa hakutoa ahadi ya kuja na viongozi na pia hakuna masharti aliyopewa kwa sababu alifuata taratibu zote za kujiunga Chadema.

“Mbona mwaka 1995 yeye (Dk. Slaa) alipokatwa na CCM na kuhamia upinzani hakupewa masharti wala kubaguliwa?

“Katiba ndiyo inayotoa utaratibu wa mtu kujiunga na chama sasa yeye ni nani mpaka awe juu ya Katiba ya Chadema? Mbona yeye hakubaguliwa na aliendelea kufaidika hadi akagombea urais?” alihoji Mbatia.

Kuhusu kauli kwamba Dk. Slaa alikuwa hajaomba wala kuteuliwa na chama chake kugombea urais, Mbatia alisema kabla ya kuingia   Lowassa Ukawa, tayari Chadema kilikuwa kimekwisha kumteua Dk. Slaa kuwa mgombea ambaye angepambana na wenzake kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) na NCCR.Mageuzi.

“Si kweli kwamba Dk . Slaa hakuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea urais, bali chama chake kilikwisha kumteua na yalipojitokeza majina ya Profesa Ibrahim Lipumba na Dk. George Kahangwa, alisema yeye ndiye mwenye vigezo vyote vya kuteuliwa kuwa mgombea wa umoja huu.

“Tulifanya vikao mbalimbali kikiwamo tulichofanya nyumbani kwa Profesa Lipumba lakini hatukufikia muafaka, lakini baada ya Lowassa kujiunga tulimwomba kwa pamoja agombee urais.

“Sababu iliyotufanya tumshawishi Lowassa agombee nafasi hiyo ni nyota yake ya siasa aliyonayo. Je, haya mafuriko tunayoyapata na tuliyopata pale Jangwani tungeyapata?

“Hizo tuhuma za ufisadi wanazozitoa juu ya Lowassa …tukianza kuwataja kwa masakata yaliyotokea katika uongozi wa Rais Kikwete (Jakaya) hakuna hata mtu mmoja atakayebaki.

“Sakata la EPA, BoT (Benki Kuu), Deep green, Richmond, vichwa hewa vya treni… hakuna atakayebaki msafi. Hivyo ufisadi si mtu bali mfumo,” alisema Mbatia.

Alisema mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, anaweza kueleza namna alivyosimamia uuzwaji wa nyumba za serikali.  Je, huo siyo ufisadi?

Mbatia alisema   wale wanaotaka mdahalo na Lowassa si saizi yake bali yeye ndiye anaweza kupambana nao.

Alimtaka Waziri wa Uchukuzi, Samueli Sitta, kuwaeleza Watanzania fedha za serikali alizotumia kujengea nyumba ya Spika kule Ulambo wakati akijua usipika ni kazi ya muda tu

Mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa Awamu ya Tano, ataunda tume tatu ikiwamo ya kuchunguza upya sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili ambalo utekelezaji wake ulilalamikiwa na wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda mkoani hapa, Lowassa alitaja tume nyingine kuwa ni za kuchunguza mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa la Efatha na wananchi na mgogoro kati ya wakulima.

“Kuhusu Operesheni Tokomeza wananchi wengi wamekuwa wakija kuniona na kunieleza wazi kuwa licha ya madhara yaliyojitokeza katika operesheni hiyo hawakulipwa, pia walipoteza haki zao, ndugu na mifugo."

Lowassa aliyetokea Namanyere alikofanya mkutano mwingine wa kampeni, aliwataka wananchi kuichagua Ukawa, kwa maelezo kuwa umoja huo utaleta mabadiliko.

Operesheni Tokomeza Ujangili ilibuniwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kupambana na ujangili ambao ulikithiri hadi taasisi za kimataifa kuingilia kati.

Hata hivyo, ilisitishwa Novemba Mosi, 2013 ili kupisha uchunguzi wa malalamiko yaliyojitokeza, yakiwamo ya wananchi kuuawa, kuteswa na kuporwa mali zao. 
 
Uchunguzi huo ulifanywa na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na sakata hilo lilipowasilishwa bungeni na kamati hiyo, lilisababisha mawaziri wanne kushinikizwa na Bunge kujiuzulu, kutokana na kuhusishwa na yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo.

Mawaziri waliong’oka ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Hamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Dk Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).

Hata hivyo, hivi karibuni Ikulu iliwaondolea doa mawaziri hao kutokana na ripoti ya Tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo kwa maelezo kuwa waliwajibika kisiasa na hawakuhusika moja kwa moja na vitendo hivyo na hakuna hatua inayostahili kuchukuliwa dhidi yao.
 
 Kuhusu mgogoro wa kanisa la Efatha na wananchi alisema: “Suala hili linalalamikiwa sana na kwa muda mrefu linawatesa wakulima na wawekezaji. Katika kuwalinda wakulima wadogowadogo itaundwa tume ili kuchunguza suala hili ili hatua za haraka zichukuliwe.”

“Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi kati ya wakulima na wafugaji, hasa waliopo katika Bonde la Mto Rukwa. Nitaunda tume ili kuhakikisha kuwa naondoa migogoro hii ambayo imedumu kwa muda mrefu,” alisema.

“Serikali yangu itanunua mahindi kwa wakulima na itawalipa riba. Haya ndiyo mabadiliko ninayoyataka. Wanaosema hawana sera wanajidanganya sana nawaambieni mkinipa kura nikaingia Ikulu wataisoma namba,” alisema.

Mbowe: Tumeunganisha nguvu
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Tumeunganisha nguvu za Watanzania wenye dhamira na mapenzi mema wanaotaka kuona mabadiliko ya nchi yetu. Tumempokea Lowassa kwa sababu tunaamini atatusaidia safari yetu ya kuwakomboa Watanzania.

“ Mgombea (Lowassa) ameteswa sana CCM na ndoto yake ya uongozi ilikuwa siku nyingi, lakini CCM hawakuiona hiyo na wakampuuza kwa maneno ya uongo.”

Mbowe alisema Rais Kikwete alimtosa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa urais na kushangazwa na kitendo cha Pinda kuendelea kubaki CCM.

Mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Lowassa nao walichukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM, lakini baada ya kutopitishwa kuwania urais walihamia Ukawa.

Kada mpya wa Chadema, Hamis Mgeja alisema: “Miradi ambayo Magufuli (Dk John) alishindwa kuijenga kwa ubora itajengwa na kumalizwa chini ya utawala wa Lowassa.

WANACHAMA zaidi ya 100 wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF wameandamana mjini Arusha na kuchoma moto bendera na kadi za vyama hivyo, wakimuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Watu hao waliandamana jana na maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada ya Dk Slaa kutangaza hadharani, Dar es Salaam kuwa ameachana na siasa.

Wakiwa katika maandamano yaliyoambatana na kubeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wanachama hao wengi wao wakiwa vijana, walijiunga na Chama cha ACTWazalendo, wakidai kuwa hawawezi kuviunga mkono vyama vyao vya zamani kwa kuwa vimenunuliwa na mafisadi.

Huku wakiimba nyimbo za kuvishutumu vyama vyao vya zamani (Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF), vijana hao walidai kuwa hawako tayari kuendelea kuviunga mkono vyama hivyo kwa sababu vimeonesha wazi kuwa havina ajenda ya kuwasaidia Watanzania masikini, bali vinawakumbatia matajiri na hivyo kupoteza mwelekeo wa kisiasa.

Mmoja wa viongozi wa maandamano hayo, Hassan Juma aliyedai kuwa mwanachama wa Chadema tangu mwaka 2005, alisema chama hicho kimenunuliwa na mafisadi na kuwa hakiwezi tena kuwasemea wanyonge ambao ndio wamekuwa tegemeo lao na hivyo hawana sababu tena ya kukiunga mkno katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

“Mimi nilikuwa naamini katika sera za Chadema za kupambana na ufisadi tangu nilipojiunga nacho mwaka 2005, lakini sasa imedhihirika walikuwa wanatutumia vijana kwa ajili ya malengo yao binafsi na kwa hiari yangu nimeamua kuachana nacho na nataka kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo ambao ni tegemeo la wanyonge hivi sasa nchini,” alisema Juma akiungwa mkono na wenzake wakiwa katika ofisi za ACTWazalendo Arusha.

Mwanachama wa NCCR-Mageuzi aliyejitambulisha kwa jina la Eliphas, alisema viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekuwa na tabia ya kuwaburuza kwa kufanya maamuzi ya kuwanufaisha wao wenyewe na hilo limewachefua na wameamua kuachana na chama hicho ili kujiunga na chama chenye mwelekeo unaofanana na watu wa chini.

“Kwa hali ilivyo hivi sasa ndani ya Ukawa ni afadhali hata kule CCM ambako tulikimbia zamani kwa kuwa hakuna demokrasia kabisa, viongozi wananunuliwa ovyo, hatuna ajenda ya kuisimamia sasa ni bora tuachane na walanguzi hao wa kisiasa na tuungane na vyama ambavyo tunaona wazi kwamba vitatetea maslahi yetu.
 
 “Hatuwezi tukalaani ufisadi ukiwa ndani ya CCM halafu ukija kwetu tunaukumbatia na kuuhalalisha. Tuliondoka CCM kwa sababu ya ufisadi na mizengwe na sasa tunaona kwamba viongozi wetu wameyakaribisha na kuyakumbatia bila aibu yoyote mambo hayo na kamwe hatukubaliani na hilo na ndio maana tunaondoka na wenzetu wengine wengi wapo njiani kutufuata,” alisisitiza Eliphas huku akichoma moto kadi yake ya NCCR-Mageuzi.

Miongozi mwa maneno yaliyoandikwa katika mabango waliyobeba wanachama hao ni pamoja na ‘Mbowe ameuza chama chetu kwa fisadi Papa,’ ‘Lowassa angekuwa mwanao amelawitiwa ungemwachia Babu Seya?’ na Bye bye Chadema, bakini kwa mafisadi wenu.’

Hata hivyo, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema vijana hao ni mamluki waliopangwa na CCM na kwamba wana taarifa za mikakati ya kuwanunua vijana ili waandamane wakionesha kuwa wanaipinga Chadema wakati ni mamluki tu wa kisiasa ambao hawana chochote zaidi ya kuganga njaa

Monday, September 1, 2014

Wapenzi na wanandoa wengi hivi leo wanapoingia kitandani tayari kwa kuianza safari ya kupeana haki zao za msingi hushindwa kufurahia tendo na hasa hali hii hujitokezwa kwa wanawake kwani mwanaume huwa na haraka iliyopitiliza!



Mwanaume atamkumbatia na kumbusu mwanamke kwa muda mfupi na kabla hata hamasa ya mapenzi ya mwanamke ahaijashika hatama, atamwingilia na ndani ya dakika sekunde ama dakika zisizozidi 3, mwanamme hufika mshindo.

Katika hali ya kusikitisha baada ya mwanaume kujitosheleza hujongea pembeni bila kujali mwenza wake hajafika mwisho wa safari hali inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya tendo endapo endapo tabia hiyo ya mwanaume itaendelea.

Kunahatua nne muhimu ambazo wapendanao wakizishika na kuzitekeleza ipasavyo basi watafanikiwa kujitosheleza kila wanapokutana na kwa hakika watakuwa miongoni mwa watu wachache wanaofurahia faragha kila wakutanapo!

Hatua ya kwanza ni kusameheana:Wanandoa wengi hushindwa kupata raha ya mlo wa usiku kutokana na kushindwa kumaliza tofauti zao kabla ya giza halijaingia, mgogoro wowote baina ya wapendanao ni lazima umalizwe kabla ya kukutana kwa ajili ya mlo wa usiku. Hii husaidia kuondoa kinyongo miongoni mwao na kuwafanya mioyo yao igubikwe na upendo ambao humfanya ahamasike kunako majambo!

Hivyo basi endapo unataka kufurahia mambo fulani hakikisha unamaliza tofauti, ombaneni msamaha na samehaneni kwa dhati kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia muwapo faragha kufurahia kile mnachokifanya kwa kuwa mtakuwa mmemalzia tofauti zenu.
Hatua ya pili ni mchezo ya mahaba:Mashamsham hunoga na kupamba moto kiasi cha kumfanya yoyote aliye kwenye uwanya wa raha kusahau kwa muda shida na matatizo yanayomuandama pale anapokutana an mtu anayeweza kumpagawisha kwa michezo ya mahaba kabla ya kuianza safari yenyewe!
Michezo hii husaidia kuamzsha hamasa na muhemko baina ya wapendanao, hivyo ili wapendanao waweze kufika mwisho wa safari pamoja na kila mmoja alidhike na udereva wa mwenzake uliowafikisha safari yao lazima watumiye muda wakutosha katika michozo yakimahaba!

Hata hivyo kila mmoja wenu anapaswa kuujua mwili wa mwenza wake. Mwili wa mwanaume ni rahisi kuuelewa kwani una sehemu moja kuu ambayo ni kama kiini cha muhemko na msisimko wa mapenzi. Sehemu hiyo ni uume. Hivyo endapo mwanamke yoyote atatumia muda wakutosha kuhangaika na sehemu hiyo basi mambo huwa safi kwa upande wa mwanaume.
Mwili wa mwanamke una shughuli pevu kubaini sehemu zenye ambazo huamsha hisia za mapenzi na ndiyo maana wanaume wengi hushindwa kuwafikisha mwisho wa safari wapenzi wao. Kiini cha hisia za mapenzi kwa mwanamke ziko kwenye kipegere G (namaanisha critoris wadu, haya ni mambo ya infenizimu tu). Kipegere G kipo nje ya uke ambapo wataalamu hudai kuwa kipo sentimita 4 kutioka ukeni.

Wanaume wengi wanaelewa hili lakini walio wengi wamegubikwa na imani potofu kuwa, kwa kuingiza kidole ukeni watafanikiwa kuinua hamasa ya za wenza wao kutaka kuanzisha safari jambo ambalo si kweli, kwani wanawake wengi hujisikia vibaya kuingizwa vidole ukeni kutokana na ukweli kwamba kucha zinabeba uchafu na bakteria wengi ambao huwasababishia kupata fangasi!
Hivyo basi, endapo wewe ni miongoni mwa wanaume waliokuwa wakiaminin dhana hii nataka nikujulishe kuwa, ukitaka kumpa msisimko uliotukuka mwenza wako usiangaike kuingiza kidole chote ukeni badala yake hakikisha unatumia kidole chako (hakikisha si kikavu) kucheza na sehemu ya nje ya uke ambapo utakutana na kipegere G na lips za ndani. Hata hivyo usisahamu kuhangaika na uke pia lakini hasa shughulika na sehemu za nje!

MUHIMU KUJUA: Mwanaume huahamasika kwa sekunde kadhaa lakini mwanamke humchukua takriban dakika 20 kuweza kuamsha hisia zake na kumfanya awe tayari kwa kuianza safari! Hivyo, mwanaume mwenye busara yaani asiye mbinafsi huakikisha anatumia muda wakutosha kumuuanda mwenza wake kabla ya kuanza safari! Hivyo mwanaume anapaswa kunza michezo ya mahaba kwa kuzingatia hatua tatu muhimu ambazo ni:-
Sehemu ya juu:

Wanume wengi kutokana ana haraka zao hukimbilia sehemu ya chini ya mwili wa mwanamke na kuacha s............... itaendele
a


 

Saturday, August 30, 2014

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/08/ue-546x291.png
MABINGWA wa England, Manchester City wamepangwa kundi moja na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na CSKA Moscow na Roma, wakati Liverpool wao wamepangwa na mabingwa watetezi, Real Madrid.
Mabingwa mara tano Ulaya, Liverpool mbali na kupangwa na mabingwa mara 10 wa taji hilo, Real pia wapo na Basle na Ludogorets.
Arsenal, imepangwa na Borussia Dortmund pamoja na Galatasaray na Anderlecht katika Kundi D, wakati Chelsea imepangwa na imepangwa na wakali wengine wa Ujerumani, Schalke, Sporting Lisbon na Maribor.
Usikose uchambuzi makini wa makundi yote katika mtandao huu. Yafuatayo ni makundi yote nane ya michuano hiyo msimu wa 2014/15
KUNDI A
Atletico Madrid
Juventus
Olympiakos
Malmo
KUNDI B
Real Madrid
Basle
LIVERPOOL
Ludogorets
KUNDI C
Benfica
Zenit St Petersburg
Bayer Leverkusena
Monaco
KUNDI D
ARSENAL
Borussia Dortmund
Galatasaray
Anderlecht
KUNDI E
Bayern Munich
MANCHESTER CITY
CSKA Moscow
Roma
KUNDI F
Barcelona
Paris St-Germain
Ajax
Apoel Nicosia
KUNDI G
CHELSEA
Schalke
Sporting Lisbon
Maribor
KUNDI H
Porto
Shakhtar Donetsk
Athletic Bilbao
Bate Borisov

Friday, May 23, 2014

Amakweli dunia imekwisha! Watu wa Dar es Salaam wanasema uzee mwisho Chalinze, Dar es Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita baada ya mmiliki wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na mfanyakazi wake aitwae Tina.
Bosi huyo na mfanyakazi wake walinaswa na mchumba wa Tina aitwae Salum Mbonde ambaye alipenyezewa umbeya huyo na mteja mmoja aliyekodi chumba kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.

Baada ya mchumba wa Tina kupewa umbeya huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati za kuchepuka aliwawekea mtego na kuwashirikisha waandishi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na askari wa doria.

BOSI ATOA SHINGO KUCHUNGULIA NOMA
OFM na mchumba wa Tina wakiwa wamelizingira eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17 usiku kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi chumba kwa ajili ya kazi maalum aliwatumia ujumbe mapaparazi wa OFM kuwa mzee Makelle aliyekuwa kwenye chumba chake alitoa shingo kama mara tatu na kuangalia kulia na kushoto kama kulikuwa na mtu aliyemuona.
APIGA HATUA ZA KUNYATA
Ilipotimu saa 8:31, Mzee Makelle akiwa tumbo wazi na kipensi chake aliangalia tena kama hakukuwa na noma, akachomoka chumbani kwake fastafasta kwa hatua za minyato na kuzama chumba namba 104 alimokuwa Tina.

SHAAABASH... WANASWA KITANDANI
Shaaabash... baada ya dakika chache OFM na mchumba wa Tina walizama kwenye chumba hicho na kuwakuta wawili hao wakiwa kitandani huku Tina akiwa na nguo za ndani.

Walipohojiwa na OFM Tina alikuwa akilia na kumuomba radhi mchumba wake na kusema bosi wake huyo ndiye alimshawishi kuchepuka naye aliona kitendo cha kumnyima kingesababisha apoteze ajira yake ambayo anaitegemea.

Mzee Makelle alipohojiwa, katika hali ya kustaajabisha baada ya kujitetea alianza kumchongea Tina kwa mchumbaake akidai si mwaminifu.

“Wewe kama huyu ni mchumba wako hilo mimi nilikuwa silijui, lakini huyu mwanamke juzi tu kalala na mwanaume mwingine palepale gesti na kama unabisha twendeni nikawaoneshwe kitabu cha wageni muone jina lake na la huyo bwana,” alisema mzee huyo.

Waungwana waliokuwa wakimsikiliza mzee Makelle walimtafadhalisha kutozungumza maneno ya kichochezi na kumtaka ajitete mwenyewe.

Baada ya sakata hilo kijana huyo alimchukua mchumba wake na kuondoka naye ambapo OFM ilifuatilia na kubaini kuwa bado msichana huyo anaendelea kufanya kazi kwenye gesti hiyo.

Endapo mfanyakazi huyo atafukuzwa kazi na bosi wake baada ya kufumaniwa OFM inaiomba serikali kuingilia kati ili mwanamke huyo apate haki zake kwani bosi huyo awali alikuwa akisema huenda katika mchongo wa kumnasa Tina anahusika.
Stori: Richard Bukos na Issa Mnally,GPL >