

Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt
John Pombe Joseph Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli
wakibadilishana mawazo na Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria TB Joshua
mara baada ya kuwasili nchini jioni hii.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini
Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini
Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano
Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini
Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni . (Picha na Freddy Maro)
*****************
Mtume TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria
ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais
wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa
uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.
TB Joshua amempongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt. Magufuli kama
mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa
Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
0 comments:
Post a Comment