Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia.
Akizungunza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na
hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
Mwambene
amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia
mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili
kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.
“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,” amesema Mwambene.
Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
“Mkapa
yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais
mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema Mwmbene na kuongeza.
Serikali
italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu
mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.
Amesema
kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi
wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi
hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.
0 comments:
Post a Comment