WANACHAMA zaidi ya 100 wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF wameandamana mjini Arusha na kuchoma moto bendera na kadi za vyama hivyo, wakimuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.
Watu
hao waliandamana jana na maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada
ya Dk Slaa kutangaza hadharani, Dar es Salaam kuwa ameachana na siasa.
Wakiwa
katika maandamano yaliyoambatana na kubeba mabango yenye ujumbe
mbalimbali, wanachama hao wengi wao wakiwa vijana, walijiunga na Chama
cha ACTWazalendo, wakidai kuwa hawawezi kuviunga mkono vyama vyao vya
zamani kwa kuwa vimenunuliwa na mafisadi.
Huku
wakiimba nyimbo za kuvishutumu vyama vyao vya zamani (Chadema,
NCCR-Mageuzi na CUF), vijana hao walidai kuwa hawako tayari kuendelea
kuviunga mkono vyama hivyo kwa sababu vimeonesha wazi kuwa havina ajenda
ya kuwasaidia Watanzania masikini, bali vinawakumbatia matajiri na
hivyo kupoteza mwelekeo wa kisiasa.
Mmoja
wa viongozi wa maandamano hayo, Hassan Juma aliyedai kuwa mwanachama wa
Chadema tangu mwaka 2005, alisema chama hicho kimenunuliwa na mafisadi
na kuwa hakiwezi tena kuwasemea wanyonge ambao ndio wamekuwa tegemeo lao
na hivyo hawana sababu tena ya kukiunga mkno katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka huu.
“Mimi
nilikuwa naamini katika sera za Chadema za kupambana na ufisadi tangu
nilipojiunga nacho mwaka 2005, lakini sasa imedhihirika walikuwa
wanatutumia vijana kwa ajili ya malengo yao binafsi na kwa hiari yangu
nimeamua kuachana nacho na nataka kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo ambao
ni tegemeo la wanyonge hivi sasa nchini,” alisema Juma akiungwa mkono na wenzake wakiwa katika ofisi za ACTWazalendo Arusha.
Mwanachama
wa NCCR-Mageuzi aliyejitambulisha kwa jina la Eliphas, alisema viongozi
wakuu wa vyama hivyo wamekuwa na tabia ya kuwaburuza kwa kufanya
maamuzi ya kuwanufaisha wao wenyewe na hilo limewachefua na wameamua
kuachana na chama hicho ili kujiunga na chama chenye mwelekeo unaofanana
na watu wa chini.
“Kwa
hali ilivyo hivi sasa ndani ya Ukawa ni afadhali hata kule CCM ambako
tulikimbia zamani kwa kuwa hakuna demokrasia kabisa, viongozi
wananunuliwa ovyo, hatuna ajenda ya kuisimamia sasa ni bora tuachane na
walanguzi hao wa kisiasa na tuungane na vyama ambavyo tunaona wazi
kwamba vitatetea maslahi yetu.
“Hatuwezi tukalaani ufisadi ukiwa ndani ya CCM halafu ukija kwetu tunaukumbatia na kuuhalalisha. Tuliondoka CCM kwa sababu ya ufisadi na mizengwe na sasa tunaona kwamba viongozi wetu wameyakaribisha na kuyakumbatia bila aibu yoyote mambo hayo na kamwe hatukubaliani na hilo na ndio maana tunaondoka na wenzetu wengine wengi wapo njiani kutufuata,” alisisitiza Eliphas huku akichoma moto kadi yake ya NCCR-Mageuzi.
“Hatuwezi tukalaani ufisadi ukiwa ndani ya CCM halafu ukija kwetu tunaukumbatia na kuuhalalisha. Tuliondoka CCM kwa sababu ya ufisadi na mizengwe na sasa tunaona kwamba viongozi wetu wameyakaribisha na kuyakumbatia bila aibu yoyote mambo hayo na kamwe hatukubaliani na hilo na ndio maana tunaondoka na wenzetu wengine wengi wapo njiani kutufuata,” alisisitiza Eliphas huku akichoma moto kadi yake ya NCCR-Mageuzi.
Miongozi
mwa maneno yaliyoandikwa katika mabango waliyobeba wanachama hao ni
pamoja na ‘Mbowe ameuza chama chetu kwa fisadi Papa,’ ‘Lowassa angekuwa
mwanao amelawitiwa ungemwachia Babu Seya?’ na Bye bye Chadema, bakini
kwa mafisadi wenu.’
0 comments:
Post a Comment