Monday, October 14, 2013

Ufoo Saro wakati akitolewa chumba cha upasuaji kupelekwa wodini.
 Manesi wakimpeleka Ufoo wodini.
 Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro,  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake  Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa ni mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.
 Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
 Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.
  Baadhi ya waandishi na wananchi wakiwa wamekusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujua hali ya Ufoo.
Mtangazaji wa ITV na Radio One, Ufoo Saro amefanyiwa upasuaji baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi na mzazi mwenziye aitwaye Anther Mushi mapema leo. Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Ufoo alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi Annastazia Saro baada ya kutokea mgogoro baina yake na mzazi mwenziye. Katika tukio hilo, Anther alimpiga risasi na kumuua mama Ufoo kisha na yeye akajilipua kwa risasi baada ya kumpiga risasi Ufoo. Kwa sasa Ufoo amehamishiwa katika wodi ya Kibasila anapoendelea kupatiwa matibabu. Umati wa watu ulikusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi ili kujua hali ya mtangazaji huyo.

Categories: ,

0 comments:

Post a Comment