Posted By:JUNGU KUU | At:Friday, October 11, 2013
 |
Utata
umeendelea kuibuka kuhusu picha zinazosadikiwa ni za hivi karibuni
zikimwonesha Wema Sepetu na Nasib Abdul "Diamond Platnumz" katika
nyakati tofauti kwenye nchi moja huko Asia wakiwa kimahaba CHUMBANI
Picha
hizi zimehusishwa na usaliti wa Diamond kwa mpenziwe wa sasa aitwaye
Penny, na gazeti moja la udaku lilichapisha habari kuwa wawili hao
hawapo katika hali nzuri baada ya Diamond kurudiana na aliyekuwa mpenzi
wake, Wema.
Wakati
Wema akiripotiwa kuwa alikuwa China kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu
ya sikukuu yake ya kuzaliwa, Diamond aliripotiwa kipindi hicho hicho
akiwa Malaysia kwa ajili ya shughuli zake za kutumbuiza na burudani.
Swali kwa Diamond:Je umerudiana na Wema Sepetu nini kinachoendelea??
'Kumekuwa na Uvumi
na Habari nyingi sana Mitandaoni na Kwenye Media tofauti kwamba mimi na
Mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu ambacho sikweli
na taarifa hizo za uongo uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment
kwenye Account yangu ya Instagram?. Hebu tujifunze kubadilika, inamaana
watu mkiwa hamko kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki
kwa chochote? Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana Mnapenda kuona
watu wanauadui... nimuda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima
Taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo nanfaida',
|


SIJARUDIANA
NA WEMA. Lakini jana na leo swali hilo limekuja tena kwa kasi baada ya
kuonekana picha mpya za Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja katika bara
la Asia ambalo bila wasiwasi ni Malaysia ambako Diamond alikuwa
amekwenda kufanya show,kwa picha hizi ni wazi,Diamond na Wema walikwenda
kwa pamoja,katika upande wa kujitetea Leo Diamond ameandika ujumbe
akikanusha taarifa za kurudiana na Wema na kusema alikuwa akifanya movie
yake mpya inayofahamika kwa jina la #TEMPTATIONS Huu ndio ujumbe
wake'Katika moja ya Muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora
toka Tanzania basi ni hii... #TEMPTATIONS .... STAY TUNED!!!!
SOON!....#DayOne #Location.
0 comments:
Post a Comment