
ASILIMIA 60 ya
wanaume wasioweza kufanya tendo la ndoa inatokana na matatizo ya kisaikolojia.
Takwimu hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Meneja wa Mradi wa Chama Cha Elimu ya Afya ya Uzazi cha Sweden (RFSU), Dk.
Cathbert Maendaenda wakati wa semina ya siku moja ya waandishi wa habari
iliyokuwa na lengo la kuzungumzia sheria ya masuala ya uzazi na ushiriki wa
wananume. Dk. Maendaenda alisema wanaume
wanaopata tatizo hilo kutokana na magonjwa, umri na maumbilie ni asilimia 40
tu.
“Kundi kubwa la wananume wanaopata tatizo hili si kwamba ni wagonjwa bali wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia, ukiwaweka chini na kuwapatia elimu wanarudi katika hali yao ya kawaida.
“Kundi kubwa la wananume wanaopata tatizo hili si kwamba ni wagonjwa bali wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia, ukiwaweka chini na kuwapatia elimu wanarudi katika hali yao ya kawaida.
“Lakini changamoto
kubwa inayopata wanaume hawa ni kwamba hospitali zetu ninyi zimejengwa kwa mfumo
wa kutoa tiba na si ushauri nasaha kwahiyo mwanaume anaweza kwenda kule ili
kuelezea tatizo lake lakini kutokana na mazingira ya hizo OPD
anashindwa
kujielezea. 

“Matokeo yake anarudi nyumbani na kukaa na tatizo, kundi kubwa la wananume wa aina hiii wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji au kujitibu wenyewe kwa mitishamba wakiamini watapona lakini mwisho wa siku hakuna unafuu unaopatikana,” alisema Dk. Maendaenda.
Akizungumzia tatizo la usihiriki wa wanaume katika suala la uzazi alisema bado jamii ina changamoto kubwa kwasababu wanaume wanapewa haki za kufanya ngono zaidi kuliko wanawake.
“Kwenye jamii tunayoishi bado kuna tatizo kubwa, wanaume wamepewa uhuru wa kufanya ngono kuliko wanawake, mwanamke akimfumania mke wake jamii na familia inachukulia jambo hilo ni la kawaida.
“Lakini mwanaume anapokwenda kushitakiwa kwao au ukweni akisema nimemfumania mke wangu na mwanaume mwingine mwanamke huyo ataonekana nuksi na jamii itamtenge
“Sasa wote huu ni
ukatili na kuminya haki za wanawake, ndiyo maana unaona mwanamke hata akijua
mume wake anatoka nje ya ndoa ataishia kulalamika mwenyewe lakini hajui hatua za
kuchukua,”alisema Dk. Maendaenda.
Alisema kutokana na hali hiyo ya kukandamizwa kwa haki zao, wanawake wengi waliko ndani ya ndoa wanashindwa kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kutokana na kuwaogopa waume zao.
Alisema kutokana na hali hiyo ya kukandamizwa kwa haki zao, wanawake wengi waliko ndani ya ndoa wanashindwa kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kutokana na kuwaogopa waume zao.
0 comments:
Post a Comment