Friday, April 26, 2013



WATANZANIA leo wanaadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Muungano huo ulisainiwa na waasisi wa mataifa hayo, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika, hayati Aman Abeid Karume aliyekuwa Rais kwa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
 
Zoezi la kutiliana saini ya kuuunganisha nchi hizo mbili na kuzaliwa nchini moja Tanzania, ilifanyika tarehe 26 April mwaka 1964 kisiwani Zanzibar na tangu hapo kukawa na Serikali mbili ndani ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri wa Muungano.
 
Mpekuzi  inawatakiwa watanzania wote popote walipo duniani maadhimisho mema ya sherehe ya Muungano na Mungu awasaidie waweze kudumisha Muungano wao na kuishi kwa amani na upendo kama ilivyokuwa dhama ya waasisi wa jambo hilo.
Categories:

0 comments:

Post a Comment