
Ni wabunge machachari wa CHADEMA kuwa mwiba mkali kwa CCM hapo jana na kuzua tafrani hasa pale naibu spika wa Bunge kuamuru Mbunge wa Singida Mashariki mh. Tundu Lissu atolewe nje baada ya kuomba utaratibu wa spika wakati mbunge nchemba akiongea na naibu spika kukataa.
Na baadae kumhoji Lissu kwanini anasimama na anaongea sana na iweje awe yeye tu, na kumwamulu atolewe nje na kugoma ndipo maamuzi hayo yakatolewa na spika wa bunge.
Chanzo za kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo, Nchemba hakuweza kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika kukatisha mkutano wa Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo, tayari wabunge hao walikuwa wameshatolewa nje baada ya askari kuongezwa.
0 comments:
Post a Comment