Monday, April 15, 2013


MKAZI wa Kijiji cha Karema mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda mkoani Katavi, Jonas Ndegela (63) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa dada yake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo alikana shitaka na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alilazimika kuahirisha shauri hilo hadi hapo Aprili 25 mwaka huu litakapotajwa tena .
Pia hakimu huyo aliamuru mshitakiwa huyo arudishwe rumande baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo.

Awali, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mwijo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 6 mwaka huu, saa 5 asubuhi kijijini Mnyamazi Kata ya Mapanda ndogo katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku moja kabla ya tukio hilo mshitakiwa alifika nyumbani kwa dada yake ambaye ni mama wa mtoto huyo anayeishi kijiji hicho cha Mnyamasi ili kumsalimia kwa kuwa walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Mwijo, baada ya Ndegela kufika nyumbani hapo kwa dada yake na kusalimiana naye, aliondoka kwenda kwenye kilabu cha pombe za kienyeji kijijini humo ambako alikunywa pombe hadi alipozidiwa na kisha kulala kilabuni humo.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa baada ya kuamka klabuni humo alfajiri ya siku iliyofuata alielekea nyumbani kwa dada yake ambako alifanya unyama huo huku dada yake akiwa kisimani akichota maji.

0 comments:

Post a Comment