


Japokuwa kuna wasiwasi kama nyota huyo
atacheza mechi ya ufunguzi ya kundi D dhidi ya Costa Rica juni 14
kwenye uwanja wa Estadio Castelao, Suarez anatazamiwa kuwa fiti kabla ya
mashindano kuanza.
"Nawashukuru wote kwa sapoti yenu," aliwaambia La Ovacion akiwa nchini kwake Uruguay.
"Nitajitahidi na kufanya maandalizi kwa bidii siku zijazo ili kuwa fiti kwa asilimia 100 na kuwasaidia wachezaji wenzangu".
Hizo ni habari njema kwa taifa hilo la
America kusini ambalo lilifika hatua ya nusu fainali ya michuano
iliyopita ya kombe la dunia nchini Afrika kusini.
Mama yake Suarez, Sandra Diaz alifurahi baada ya zoezi za upasuaji kufanikiwa.
Alisema: ‘upasuaji umekamilika na
tunamshukuru Mungu kila kitu kimekwenda vizuri. Tatizo la Luis halikuwa
kubwa sana kama tulivyodhani"
0 comments:
Post a Comment