Anachunguzwa: Moyes alikuwepo kwenye baa mjini Clitheroe wakati anatukanwa.
KOCHA wa zamani wa
Manchester United, David Moyes anahojiwa na polisi kwa tuhuma za
kumshambulia kijana mmoja kwenye baa moja ya pombe kwa madai ya kuchekwa
baada ya kupoteza kazi.
Kocha
huyo mwenye miaka 51 alimrithi Sir Alex Ferguson, Old Trafford, lakini
alimaliza miezi tisa tu na alimshambulia kijana huyo baada ya
kukashifiwa na kijana huyo maeneo ya Emporium, mjini Clitheroe.
Kijana huyo aliyeshambuliwa na Moyes ana miaka 23 na jina lake ni Joshua Gillibrand.
Tukio: Joshua Gillibrand anadai alishambuliwa majira ya saa 10:00 usiku wa jana jumatano.
Inasemekana Moyes alikerwa na kijana
huyo mlevi aliyemtukana kocha huyo baada ya kufukuzwa kazi hivi karibuni
na kumuita 's*** (hatujaona haja ya kutafsiri kimaadili), akimaanisha
hajawahi kushinda kombe, alisema shahidi.
Baada ya maneno hayo vurugu ziliibuka mezani ambapo glasi zote zimeanguka chini.
Mr
Gillibrand, alikula vibao na alichubuka kwenye bega kutokana na ugomvi
huo, lakini hakuhitaji kwenda hospitali kupata matibabu zaidi.
Leo polisi walithibitisha kufungua uchunguzi juu ya tukio hilo na wanatarajia kuongea na kocha huyo wa zamani wa Everton.
Maeneo ya fujo: Baa ya wine ya Emporium wine, mjini Clitheroe, Lancashire, ambapo kulitokea tukio hilo
Huyu ndiye Mr Gillibrand aliyekula kisago kutoka kwa David Moyes
0 comments:
Post a Comment