Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

Monday, October 14, 2013


0
Kutana na tweets za mkali wa comedy kutoka Orijino Komedi Mpoki a.k.a Mwarabuwadubai ambapo hizi ni baadhi tu ya tweets amewahi kuziandika kwenye page yake ya twitter na unaweza kumfata pia kupitia @mwarabuwadubai
2
3
4
5
6
7
9
10
11
12
13
14
15
16




Saturday, October 12, 2013

Huyu  ni  Msanii  mkongwe  maarufu  kwa  jina  la  Ray  C ambaye  leo  hii  ameamua  kuyanadi  mapaja  yake  akidai  kwamba  hiyo  ndo  sehemu  muhimu  ya  mwili  wake...Kila  mwanamke  ana  mvuto  wake, wapo  wanaojivunia  nyuso  zao  zenye  macho  yaliyoumbwa  yakaumbika, nyuso  zisizo  na  chunusi  wala  aina  yoyote  ya  kovu...Wapo  pia  wanaojivunia  makalio  yao  na  sote  tumekuwa  tukishuhudia  jitihada  mbali mbali  za  akinadada  za  kujitengenezea  makalio  ya  bandia ( ya  kichina ) ili  kujiongezea  mvuto  kwa  wanaume.

Hali  ni  tofauti  kidogo  kwa  msanii Ray C.Yeye  anaamini  kwamba  mapaja ndo  kila  kitu  na  kwamba  ni  hicho kigezo  muhimu  kinachoangaliwa  na  wanaume  wengi wa  siku  hizi...

"Nani  asiyejua  kwamba  kuna  makalio  ya  kichina? Umewahi  sikia  wapi  mapaja  ya  kichina?..Haya  tunayo  wachache  ambao  tumejaliwa  na  muumba  wetu".Hii  ni  kauli  ya  Ray  C alipokuwa  akipiga  stori  na  mpekuzi  wetu.
Akongelea kuhusu  afya  yake  kwa  ujumla, Ray  C amewashukuru  kwa  mara  nyingine  watanzania  wote  waliokuwa  naye  wakati  wa  akiwa  mgonjwa."Sitachoka  kuwashukuru  watanzania  wenzangu  ambao  walikuwa  pamoja  nami  pindi  nikiwa  mgonjwa. Nguvu  zangu  kwa  sasa  nimezielekeza  katika  kuiimarisha  afya  yangu  na  ndo  maana  unaniona  niko  hivi  kwa  sasa.

"Haikuwa  kazi  nyepesi  kuirejesha  afya  yangu  ndani  ya  muda  mfupi.Nilidhani  mapaja  yangu  hayatarejea  tena  katika  hali  yake.Mungu  ni  mwaminifu, kila  kitu  kiko  vizuri  kama  nilivyokuwa  nataka"..Ray  C

Friday, July 26, 2013



LILE sakata la staa wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya kutuhumu kumshika ugoni staa mwenzake aliyemtoa kwenye gemu, Lucy Francis Komba limeingia sura nyingine kuafutia picha za filamu inayodaiwa kuchezwa na wawili hao kunaswa na Ijumaa, twende hatua kwa hatua. 
Katika baadhi ya matoleo ya Magazeti ya Global Publishers zilichapishwa habari za mastaa hao kuzua bifu zito kufuatia Lucy kumchukua mwanasoka wa Rwanda ambaye ni mume wa ndoa wa Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ na kucheza naye filamu jambo ambalo Uwoya alilipinga.
KWA NINI UWOYA ALIPINGA?
Uwoya alipinga mumewe kushiriki filamu hiyo kwa sababu aliambiwa washiriki ni wawili tu, mumewe Ndikumana na Lucy. Filamu inaitwa Kwa nini Nisimuoe?
Kwa mujibu wa Uwoya, hajawahi kuona filamu ya kawaida inachezwa na watu wawili tu, akasema Lucy alitumia nafasi hiyo kuwa na mumewe kimapenzi.
Hata hivyo, Uwoya alisema akiviona vipande vya picha za filamu hiyo atajua ukweli.
Wiki iliyopita aliviona vipande hivyo na kuweka msimamo wake kwamba hakuna filamu ni mapenzi tu.

IJUMAA LAFUKUNYUA, LAIBUKA NA PICHA
Kama kawaida ya Magazeti ya Global Publishers, liwe Ijumaa, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Amani, Championi au Risasi ni kuchimba mambo kwa undani na kuupata ukweli wa jambo, hivyo timu ya wanahabari wetu ilizama mitaani na kuzisaka picha za filamu hiyo.
Julai 23, 2013, Ijumaa lilifanikiwa kuzipata picha hizo ambazo moja baada ya nyingine zinawaonesha Lucy na Ndikumana wakiwa katika mapozi mbalimbali ndani ya filamu (angalia picha).

MWANZO, MWISHO NI WAWILI TU!
Katika picha hizo ambazo ziko mikononi mwa dawati la Ijumaa, wasanii walioonekana ni Lucy na Ndikumana tu hivyo kushibisha yale maswali ya Uwoya kuwa ni kwa nini filamu nzima ichezwe na watu wawili tu?

HADITHI YA FILAMU YADAIWA NI KISA CHA KWELI CHA UWOYA NA NDIKU
Habari za hivi karibuni zilisema kuwa,   cha ajabu, kisa kinachosimuliwa katika filamu hiyo ni cha kweli.
Ilidaiwa kuwa kisa hicho kilimpata Ndiku baada ya kukutana na Uwoya kwa mara ya kwanza kabla ya kufunga ndoa.
Madai hayo yanaongeza chachu katika moyo wa Uwoya na kuzidi kuamini kuna kitu kinaendelea kati ya mumewe na Lucy.

UWOYA AKATISHA ZIARA SWAZILAND
Uwoya alipotafutwa na Ijumaa juzi ili kumsikia msimamo wake kuhusu hali tete katika ndoa yake baada ya hisia zake kuwa anaibiwa mumewe na Lucy, alisema atapasua jipu atakapotua Bongo akitokea nchini Swaziland ambako alikwenda kwa ziara binafsi.
Alisema kuwa amelazimika kukatisha ziara na kurudi Tanzania kwa vile suala la Lucy na mumewe linamnyima raha kuendelea kuwepo ugenini.
“Narudi Bongo Jumatano (juzi). Unajua hili suala limeninyima raha kabisa. Siwezi kuendelea kuwepo huku ugenini. Nikifika nitatoa la moyoni,” alisema Uwoya.

LUCY AZUNGUMZA KUTOKEA DENMARK
Wakati Uwoya akizungumza kutokea jijini Mbabane, Swaziland, Lucy yeye alitoa sauti yake akiwa nchini Denmark kwenye Jiji la Copenhagen.
Alipoulizwa kuhusu tambo za Uwoya baada ya yeye kucheza filamu na mumewe Ndikumana, alijibu:
“Mimi sina cha kusema, yeye anajua mimi ni nani katika filamu. Mumewe kaonesha mapenzi ye kucheza filamu yangu, sasa anaposema ningemtaarifu yeye kama nacheza filamu na mumewe ili iweje? Kwa nini asimlaumu mume wake ambaye ndiye alipaswa kumtaarifu?” alisema Lucy.
Lucy aliongeza: Kama Ndiku angekuwa mtoto chini ya miaka kumi na nane nataka kucheza naye filamu hapo kweli, ningepaswa kumtaarifu Uwoya kama mama mtu, lakini mume, si sahihi kunilaumu.

MADAI YA HADITHI YA FILAMU KUWA KISA CHA KWELI
Kuhusu madai kwamba hadithi ya kwenye filamu hiyo ni kisa cha kweli kati ya Uwoya na Ndiku, Lucy alijibu:
“Teh! Teh! Si kweli bwana. Kama Uwoya ndiyo kasema hivyo basi ana kisa kinachofanana na cha filamu yangu. Mimi filamu ni yangu na hadithi ni yangu.”

WAONGOZA FILAMU BONGO WANASEMAJE KUHUSU WATU WAWILI TU?
Ili kujifunza juu ya wasanii wawili kucheza filamu nzima, Ijumaa liliwatafuta baadhi ya waongoza filamu Bongo.
Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’: Kusema kweli ni vigumu sana. Labda kama zile filamu za porini, mtu anakimbizwa na wanyama (documentary).
“Lakini kucheza filamu za mjini halafu wawili tu, mnagombana wenyewe mnapatana wenyewe ni kazi sana,” alisema Chuz.
Jacob Steven ‘JB’: Du! Labda kama utakuwa umekusudia kupunguza bajeti, lakini pia haitakuwa filamu nzuri, wawili tu?! Kwanza ni filamu gani hiyo ya watu wawili tu?
Ijumaa lilimkatia simu.
Mahsin Awadh ‘Dk Cheni’: Mh! Zipo kama mtu mwenyewe atakuwa ameamua, lakini sidhani kama sokoni itakubalika. Ni nani huyo kwani?
Ijumaa likamkatia simu.
Wazoefu wengi wa filamu walisema documentary ndizo zinaweza kuwa na watu wawili lakini si filamu.

Thursday, July 25, 2013


  Lady  Gaga  ametoa  kali  ya  mwaka  baada  ya  kukubali  kufotolewa  akiwa  mtupu  ili  kuupamba  ukurasa  wa  mbele  wa  gazeti  la  V magazine...

Baadhi  ya  fans  wake  wamefunguka  na  kudai  kuwa  uroho  wa  pesa  utamponza  huku wengine wakidai   kuwa  msanii  huyo  atakuwa  amekubali  kuanikwa  hivyo  ili  kuvuta  "attention"  ya  mashabiki  wake  kwa  ujio  wa  albam yake  mpya  itakayoitwa  Artpop

Albamu hiyo inatarajiwa kuwa   sokoni mwezi wa 11 na nyimbo ya kwanza kutoka kwenye  album   hiyo  itatambulishwa mwezi wa nane tarehe 19.

Wednesday, June 5, 2013


Msafara wa kupokea mwili wa msanii  marehemu Albert Mangwea ukiwa unaingia morogoro hapa ni eneo la nane nane,Umati mkubwa umejitokeza katika mapokezi hayo jioni ya leo

 
 MAPOKEZI YA MWILI WA NGWEA ENEO LA MAZIMBU ROAD KIHONDA.





Saturday, May 25, 2013




Muigizaji Tope Osoba amekataa kuwa na mahusiano bila ya kukutana kimwili, na kufunguka kwamba anashangazwa na wasanii wengi wa Tanzania na Nigeria ambao wamekuwa wakiolewa na wanaume zao na kuishi nje ya nchi kwa zaidi ya mwaka na hakuna kati yao aliyepata nafasi ya kumtembelea mwenzake.
 
“Ngono ni kitu cha kuburudishana kati ya wawili wapendanao. Ngono ni nzuri. Imeumbwa ili wapenzi wa-enjoy na kubadilishana siri za mioyo yao.” Alifunguka actress huyo.
 
Alipoulizwa kuhusu mapenzi kabla ya ndoa, Tope alisema: “Mapenzi kabla ya ndoa ni poa tu, al muradi usalama kwanza. kwanza tusidanganyane, hauwezi kudumisha uhusiano bila ngono.”
 
Alifafanua kuwa maisha ya namna hiyo hayapo na kama yapo yana kitu nyuma ya pazia kwa kuwa hakuna mwaminifu bila ya sababu ya msingi

Zile picha za kundi la Ze Komedy la linalorusha kipindi chake kupitia televisheni ya East Africa TV zinazowaonesha wasanii hao wakiwa na mabint ufukweni zimechukua sura mpya baada ya wanasheria  kuahidi kuzisaidia familia za wazaza wa mabint hao.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema" Nimeziona picha hizo kupitia mtandao wenu kweli imeniuma kama mzazi kwani huo ni unyanyasaji ambao haukubariki hata kidogo naziomba familia za mabint hao kuchukuwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kushtaki ili iwe fundisho kwa wasanii wengine wanaopenda kudhalilisha watu wengine kwa masrahi yao binafsi" Alisema Fortunatus Kasomfi ambae ni mtanzania anaeishi nchini Afrika Kusini

Aidha nae Hawamu Juma ambae ni mkazi wa Arusha maeneo ya Unga Limited ambae ni Mwanasheria maarufu Mkoani humo alioneshwa kusikitishwa sana na tukio na kuwashauri wazazi wa wasichana hao kumtafuta kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka wasanii hao
 
" Napenda kuwashauri wazazi wa wabinti hao kama wanahitaji msaada wa kisheria wanitafute kupitia  simu namba 0713-146416 nitawapa mawazo ya kitaalam ya kisheria ili wasanii hao wafikishwe mahakamani" Alisema Mwanasheria huyo

Taarifa  za  ndani ya chungu zinadai  kuwa  kulikuwa na ushawishwaji mkubwa kwa mabinti hao wakati wa kupigana picha hizo kwa madai kuwa watasaidiwa kuwa mastaa kama watapiga picha hizo na mastaa hao. 
Huyu  ni  Happy na Master  Face  wakifanya  Uchafu wao....Hapa  wanatomasana  kabla ya uzalendo kuwashinda  na  kuamua  kuvunja  amri  ya  sita...

 
Tayari kuna taarifa kuwa baba mzazi wa mmoja wa wasichana hao ambae anaishi Tabata ameanza kuchukuwa hatua za awali kwani siku ya tukio msanii wa kundi la Komedy Manaiki Sanga alifika nyumbani kwa bint huyo na kumchukuwa kwa madai kuwa anaenda nae Location.

Mpaka sasa kiongozi wa kundi hilo ambaye  ni Mtanga ameshindwa kuchukuwa hatua yoyote dhidi ya wasanii wake walihusika na tukio hilo chafu ....

Xdjayz

feza-kessy-rick-ross-vanessa-mdee
feza-kessy
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye   mitandao  mbalimbali nchini Tanzania, mrembo huyu, mwanamuziki Feza Kessy, ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2013 (BBA “The Chase.” Well, hizi ni baadhi ya picha zake

Thursday, May 16, 2013


linah-barnaba-0
Na Andrew Chale
KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’ huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia 



Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake.
Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.
“Juzi Linah, haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na ** kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuwa na hofu, na wala hakutaka kusikia ushauri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Linan, amabaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.
Hata hivyo taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu zinafuata ilizisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT na watu wa karibu wanaoiunga THT.
“Wewe nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo taarifa, sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao sie na tunaouwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.
Aidha, katika ‘ku-balance’ uhondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima simu.
Katika kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.
Shoo hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau wa burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa Lady Jay Dee na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali wanatarajia kuudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin Logiki’.
Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na wazee wa ‘kuingilia logik’ wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya watu.
Mtandao huo wa kijamii blog, ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (Ladyjaydee.blogspot.com) Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13..
**KWA TAARIFA ZAIDI KWA KINA JUU YA BARNABA NA LINAH, usikose kuzisoma katika gazeti la Tanzania Daima ** Pindi watakapopatikana tutaweka hadharani kila kitu.
Mwisho
<