Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Monday, October 14, 2013


  
 ITV journalist Ufoo Saro is wheeled out of the operating room at Muhimbili National Hospital yesterday.  Ms Saro was shot and seriously wounded by her fiance, who also shot the reporter’s mother dead before taking his own life.  
PHOTO | EMMANUEL HERMAN

Dar es Salaam. 
The family of Antel Mushi was not aware he was in the country until he shot dead his fiancee’s mother before taking his own life on Sunday, according to a close relative.

Mushi, who was working with the UN in Sudan, also shot and seriously wounded Ms Ufoo Saro at her home in Kibamba, Dar es Salaam.

His elder brother, Mr Silver Mushi, said yesterday that a friend called him on the fateful day at around 9am, and asked him whether Antel had come home from Sudan after he heard on the radio and television that he (Antel) had shot and killed Ms Anastazia Saro, 58, and seriously wounded his fiancee, who is a reporter with ITV, before turning the gun on himself.

Mr Mushi said he last spoke to Antel on October 9, this year, when the latter was travelling on official duty within Sudan.

“He told me to pray for him...we did not speak again until I was called by a friend who alerted me about the radio and television reports,” he said.

Mr Mushi said Antel, 40, was a down-to-earth person “who had more friends than enemies”.

He added that he could not have even remotely imagined that his younger brother could do what he did on Sunday.

Mr Moshi said he last saw Antel in July when he came to Tanzania on leave, and recalled that Ms Saro saw her fiance off at Kilimanjaro International when he left for Sudan.

Antel received primary education in Moshi before he went to Zanzibar for his secondary education. He joined ITV in 1994 before joining the then Arusha-based International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR).

He left ICTR and joined the UN in Sudan where he was working as a telecommunications officer.

“He liked studying a lot and was at the time of his death undertaking distance learning through a university in India, and was due to graduate in December,” Mr Mushi said.
Antel lived with Ms Saro for about 13 years and the couple had a child
 
                    Waumini wa dini ya kiisilamu wakipinga matumizi ya jina Allah kwa kikristo

Mahakama nchini Malaysia, imeamua kuwa watu wasio waisilamu wasitumie jina 'Allah' kumaanisha Mungu katika katika imani zao na kubatilisha uamuzi wa mahakama ndogo uliotolewa mwaka 2009.
Mahakama ya rufaa ilisema kuwa jina Allah linapaswa tu kutumiwa na waumini wa kiisilamu la sivyo linaweza kuzua taharuki miongoni mwa jamii.
Watu wa imani zote nchini Malaysia wanatumia neno Allah kumaanisha Mungu.
Wakristo wanateta kuwa wamekuwa wakitumia jina hilo la Allah katika lugha ya Malay na ambalo lilitokana na lugha ya kiarabu kumaanisha Mungu kwa miaka mingi na kuwa uamuzi wa mahakama unakiuka haki zao.
Mwanamke mmoja mkristo alisema kuwa uamuzi huo utaathiri jamii pakubwa.
"ikiwa tutawazuia watu wengine kutumia jila la Allah, basi itatubidi kutafsiri Bibilia nzima upya" Ester Moiji kutoka jimbo la Sabah aliambia BBC.
Umauzi ulitolewa na mahakama ndogo mwaka 2009 ulisababisha taharuki baina ya waisilamu na wakristo huku makanisa na misikiti ikishambuliwa.
Ilitokea baada ya serikali kusema kuwa jarida la kikatoliki la The Herald, haliwezi kutumia jina Allah katika makala yake ya lugha ya Malay kumaanisha Mungu kwa kikristo.
Wahariri wa jarida hilo lilikwenda mahakani kupinga uamuzi huo na mahakama ikafanya uamuzi uliowapendelea. Serikali baadaye ilikata rufaa.
Lakini katika uamuzi wake leo, jaji alisema kuwa jina Allah haliwezi kutumika kwa dini ya kikrsito kumaanisha Mungu na kuwa ikiwa jina hilo litatumiwa basi huenda likazusha taharuki baina ya jamii.
Mhariri wa jarida hilo alisema kuwa alighadhabishwa na kushangazwa sana na uamuzi wa mahakama na kwamba atakata rufaa.
Wafuasi wa jarida hilo wamesema kuwa Bibilia zilizoandikwa kwa lugha ya Malay zimekuwa zikimtaja Allah kumaanisha Mungu kwa kikristo tangu zamani sana.





....KWELI DUNIA WAWILI WAWILI.....

HUYU KIJANA AISHI KWA TABU KUTOKANA NA WATU WAMUONAPO HUANZA KUKIMBIA HUKU WENGINE WAKIMZONGA KUTOKANA NA KUFANANA SANA NA MAREHEMU STEVEN KANUMBA.


TOFAUTI na inavyoaminika na wengi kuwa watumishi wa Mungu ni watu safi, safari hii Mchungaji Obed Ntimba wa Kanisa la Anglikana Gongo la Mboto, Dar es Salaam amejikuta akivunja agano la Muumba baada ya kunaswa gesti akiwa na mke wa mtu.
 
Tukio hilo la aibu lilimkuta mchungaji huyo Ijumaa iliyopita saa saba na nusu za mchana katika gesti moja (jina lipo) iliyopo nyuma ya Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar.
 
Siku moja kabla ya tukio, makachero wetu walitonywa kuhusu dhambi hiyo na mtu wa karibu na watu hao akisema kuwa anaumia kwa sababu mchungaji huyo ana mke na watoto na mwanamke huyo, Rose ni mke wa mwanajeshi kwa hiyo aliamini tendo wanalotaka kulifanya ni uovu katika jamii.

 
Mtoa habari wetu huyo alisema tukio hilo lilipangwa kukamilika kesho yake Ijumaa katika gesti hiyo ndipo kazi ya kuwafuatilia hatua moja baada ya nyingine ilianza.
  
Ijumaa saa sita mchana, mtonyaji wetu alipiga simu  na kuweka wazi kwamba wawili hao wapo njiani kuelekea gesti, kila mmoja kwa usafiri wake.
 
Ndipo makachero wetu  walipowatonya polisi na kuambatana nao mpaka kwenye gesti hiyo na kujipanga kwa mbinu za kisasa za kutoonwa na ‘adui’.
Makachero hao  walifanikiwa kupata ramani ya chumba walichoingia wawili hao ambapo ‘rumu’ namba 1B ndiyo iliwasilishwa kwamba Rose na mchungaji wake wamo humo.
 
Saa saba na nusu mchana, Makachero wetu na polisi waliingia hadi mapokezi ya gesti hiyo kwa kificho na kutoa maelekezo kwa mhudumu. Mhudumu aliongozana nao hadi mlangoni na kugonga lakini haukufunguliwa.

 
BAADA YA DAKIKA TANO
Wakati mlango huo ukigongwa na mhudumu bila kufunguliwa, mchungaji huyo alisikika akisema na kuuliza:
“Subirini kwanza.”
“Lakini ninyi ni akina nani?”

 
Baada ya dakika tano kupita, mlango ulifunguliwa, mchungaji akakutana na macho ya timu nzima. Alipigwa butwaa asijue la kufanya huku akitetemeka, Rose alikuwa ndani ya khanga moja!
 
MCHUNGAJI MSOBEMSOBE HADI POLISI
Polisi waliwabeba msobemsobe wote hadi Kituo cha Polisi cha Urafiki-Ubungo, Dar ambapo kila mmoja alianza kujieleza.

 
MCHUNGAJI APANGULIA HUDUMA YA KIROHO
Kituoni hapo, Mchungaji Ntimba alipobanwa kuhusu sababu za kuingia gesti na mke wa mtu, alisema waliingia kwa ajili ya huduma ya kiroho kwani mwanamke huyo alikuwa anataka kufungua kanisa ndipo alipomuomba yeye amsaidie.

 
“Mimi sikuwa na lengo baya jamani. Huyu dada alihitaji kufungua kanisa, akaniambia ili nimshauri hawezi kukaa  sehemu ya wazi kwa kuwa mume wake ni mwanajeshi anaweza kuonekana na watu wakampa taarifa.
 
“Ndipo nikaamua kwenda naye katika nyumba ile ya kulala wageni kwani wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya huduma, wakitokea nchi mbalimbali huwa wanalala pale na wahusika wa pale wananifahamu sana.
 
“Baada ya kuingia gesti nilibanwa na haja ndogo, nikaenda kujisaidia. Cha kushangaza niliporudi nilimkuta huyu dada amevua nguo zote na kuanza kunishawishi lakini sikuwa na lengo hilo jamani,” alijitetea mchungaji huyo.
Baadhi ya picha zilizopo  zinamuonesha mchungaji huyo akiwa amevaa suruali lakini amesahau kufunga zipu huku kondom zikiwa pembeni kitandani!
 
MSIKIE MKE WA MTU SASA
Baada ya mchungaji kutoa maelezo yake, mke wa mtu naye alianza kutiririka ya kwake huku akionesha ushahidi wa meseji za simu ambazo mchungaji huyo alikuwa akimtumia akimshawishi kumpa penzi.

 
“Huyu mchungaji nilikwenda kwake kwa lengo la kufanya kazi kanisani lakini kuanzia hapo amekuwa akinishawishi kuwa anataka nimpe penzi ili aweze kuniweka katika sehemu nzuri kanisani.
 
“Nilikuwa nakataa, lakini akasema tukutane pale gesti tuongee zaidi. Nilikataa kukutana gesti, akaniambia pale ni ofisini, mara nyingi akiwa anaongea na waumini mambo muhimu ya huduma ya kiroho huwa anakutana nao pale.
“Nikakubali lakini kabla hata hatujaongea chochote alianza kuvua nguo zake na kuanza kunilazimisha tufanye mapenzi huku akiwa na ‘kinga’ kabisa na mimi nikavua nguo lakini kabla hajatimiza lengo lake ndipo wakaingia watu wakiwa na askari.
 
“Mimi nashukuru sana kwa sababu hawa ndiyo wameniokoa. Nilikuwa nikisikia habari za huyu mchungaji kuwa ana tabia ya kuwafanyia wasichana wengi vitendo hivyo na kweli leo ndiyo nimeamini,” alieleza mwanamke huyo.
 
Katibu wa kanisa hilo (jina halikupatikana mara moja) alimuombea msamaha mchungaji kwa waandishi huku akionesha kuumizwa na kitendo hicho baada ya kuoneshwa ushahidi na kukiri kwamba una ukweli tofauti na alivyokuwa akifikiria awali kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
-Source: Global Publisher.


Sunday, October 13, 2013




Alfajiri  ya  leo, mtangazaji  wa  ITV   anayejulikana  kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.
Akizungumza na Jungu Kuu,  kamanda Wambura  ambaye  ni kamanda  wa polisi wa  mkoa wa kipolisi wa kinondoni  amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
 
Kamanda wambura amedai  kuwa mwanaume  aliyetenda  mauaji  hayo ni  mchumba  wake  na  alikuwa anafanya  kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.

Kwa  mujibu  wa  Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili  awasuluhishe
Baada  ya  usuluhishi  kuanza  na  kuonekana  kuwa  tatizo  liko  kwa  mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa  na  mazoea  ya  kumtetea mwanae   na  ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo....
Alipomuua  mama  huyo, mwanaume huyo  alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.


Saturday, October 12, 2013

 
Msanii wa Filam Tanzania ajulikanae kwa jina la Wolper yuko hoi Hospitalini huku akiomba Dua kwa wapenzi wake wamuombee ili apone haraka. Wolper ameripot taarifa za kuumwa kwake katika akaunti yake ya facebook na kuainisha ugonjwa unaomsumbua ni Maralia na ujumbe huo umesomeka hivi: clip_image002


NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima. Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.


AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.

MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha.
MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake, wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli ya kazi za ndani.
Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano iliyopita.


Thursday, July 25, 2013



WANAFUNZI 12 wa Shule ya Sekondari ya Mlowa iliyopo Wilaya ya Iringa Vijijini wamenusurika kufa baada ya bweni walilokuwa wamelala kuungua kwa moto na kuteketeza vitu ambayo vilikuwemo ndani.  

Tukio hilo linadaiwa lilitokea baada ya hitilafu ya umeme wa nishati ya jua (Sola) iliyosababishwa na wanafunzi ambao walikuwa wamelala katika bweni hilo kuunganisha nyaya kienyeji kwa ajili ya kusikiliza redio na kusababisha hasara ambayo inakadiriwa kufikia sh. milioni 1.8.

Akizungumzia jana ofisini kwake juu ya tukio hilo la kuungua kwa bweni na kunusurika kwa wanafunzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlowa, Mwalimu Frank Mahai alisema wanafunzi wa l i o n u s u r i k a awa l i walikuwa wanaishi nje ya shule. 

 Alisema, mipango ya kuishi katika bweni hilo ilifanywa katika kikao cha wazazi na walimu kwa ajili ya wanafunzi ambao wanatoka mbali na shule ili wapate mahali pa kuishi katika muhula wa mitihani ya mwisho.


Mkuu huyo alisema kuwa, wanafunzi wengine wa shule hiyo wakati inaungua walikuwa wamekwenda kucheza mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kalenga na kubakia wanafunzi 12 katika bweni ambapo saa 1:30 jioni moto ulianza kuunguza bweni hilo.

“Wanafunzi waliohusika na kuunguza ni baada ya kuunganisha nyaya kienyeji na kusababisha shoti hadi kuunguza bweni hilo,” alisema Mkuu huyo.
Alivitaja vitu vilivyoungua kuwa ni pamoja na nguo za wanafunzi, mabegi, madaftari, magodoro pamoja na paneli za sola ambazo zimeteketea moja kwa moja pamoja na dari ya chumba cha bweni ambapo jumla ya gharama zake zinafikia kiasi hicho cha fedha.


Hata hivyo Diwani wa Kata ya Mlowa, Charles Nyagawa (CCM) akizungumzia tukio hilo alisema kuwa amesikitishwa na kuungua kwa bweni hilo ambalo wazazi walishiriki kujenga na walitumia gharama kubwa.


Diwani huyo alisema, amesikitishwa na tabia za wanafunzi kuunguza bweni hilo kutokana na kujiingiza kwenye ufundi ambao hawaujui na wala hawana utaalamu nao.
 
Al i s ema k uwa , p i a anawashukuru wazazi na wananchi ambao walifika katika kijiji hicho na kuuzima moto na kuwa i n g awa h awa k uwe z a kufanikiwa anawashukuru kwa ushirikiano ambao w a l i u o n e s h a k a t i k a kuhakikisha moto huo unazimika na kuokoa baadhi ya mabweni mengine yasiendelee kuungua moto na kuteketea mali zingine zikiwemo za wanafunzi ambao walikwenda kwenye michezo na vitabu vya shule.

Majira:

Sunday, July 21, 2013






<

Friday, May 24, 2013


INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.

Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia  katika  dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.

 

Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini. 


Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.

Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.

Haraka timu ya waandishi  wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
 
Taarifa iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya kumuondoa denti huyo.


Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.

Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.

Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.

Waandishi wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa darasani.


Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.

“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki aliniambia nije kwake.
 

“Naombeni mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.
 

Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha. 

Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.


UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
 
“Ndugu zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma (utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa anamtengenezea yule binti  wa watu maisha?).”
 
Utetezi wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada nambaWS/RB/585/2013 – KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.

 GPL 

Sunday, May 19, 2013


Mbunge  wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) hivi sasa  anaongoza  vurugu za machinga Iringa Mjini eneo la mashine tatu....
Polisi mkoani Iringa wanapambana  nao  kuidhibiti hali hiyo....
Chanzo: Wapo Radio

Saturday, May 18, 2013



Hali ya wasiwasi imelikumba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwepo kwa tetesi ya shambulio la kigaidi katika maeneo ya Bunge. 

Hali hiyo inafuatia ujumbe mfupi wa maneno uliosambazwa, ukitaadharisha kuwa kuna tukio la kigaidi limepangwa kufanywa katika eneo la Bunge.

Ujumbe huo uliosambazwa kwenye simu za baadhi ya wabunge ulisomeka hivi:-

"Kuna kikundi kina mkakati wa kufanya shambulio la bomu bungeni Dodoma na msikiti wa Msavu Morogoro. Ni ndani ya muda mfupi wakati bado vikao vya Bunge,"ailisema sehemu ya ujumbe huo.


Habari zaidi zinasema kuwa tayari jeshi la polisi imefanikiwa kupata mtu aliyetuma ujumbe huo, ambaye anadaiwa kutuma kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na wamefanikiwa kumleta mjini hapa kwa mahojiano zaidi ili kufanikisha upelelezi.



Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mussa Azzan Zungu, juzi alilitangazia Bunge hali hiyo ya hatari  wakati wabunge wakiendelea na mjadala wa hotuba ya makadirio ya matumizi wizara ya Uchukuzi ya mwaka 2013/14, na kulazimika kurudia tangazo hilo wakati akiharisha Bunge.  


“Waheshimiwa wabunge wote mnaombwa kuanzia kesho tarehe 17, mwezi huu, mwaka huu, kutoegesha magari yenu pembezoni mwa uzio unaozunguka ofisi ya bunge hapa Dodoma…Badala yake magari hayo yaingizwe katika geti la eneo la maegesho ya waheshimiwa wabunge ndani ya viwanja vya Bunge” alisema Zungu


Alisema mbunge yeyote atakaye taka kuegesha gari lake nje ya ofisi, anaombwa aegeshe ng’ambo ya upande wa kaskazini wa barabara itokayo jijini Dar es Salaam.


Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema ulinzi umeimarishwa katika eneo lote la Bunge kuhakikisha hakuna chochote cha hatari kinachoweza kutokea.

“Vijana wangu wanafanya kazi yao vyema na iwapo kuna tishio lolote lile litafanyiwa kazi,” alisema Dk Nchimbi

Dk Nchimbi alisema ulinzi utaendelea kuimarishwa katika eneo hilo kuliko wakati wowote ambao Bunge limewahi kuwekwa katika usalama.


RASIMU ya Sera ya Elimu na Mafunzo nchini inapendekeza kuunganisha elimu ya msingi na sekondari ya kawaida ya sasa ili kuunda elimu-msingi itakayotolewa kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2018, imefahamika. 


Rasimu ya kwanza ya Sera hiyo imeshakamilika na sasa wadau mbalimbali wanatoa mapendekezo yao kuiboresha, kabla ya kupelekwa bungeni ili kutungiwa sheria.


Aidha, mikakati hiyo itakayotekelezwa ni kuhuisha muundo na utaratibu mpya wa elimu na mafunzo kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na mitano anapitia elimu ya awali kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja kabla ya kujiunga na elimu-msingi.


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alithibitisha kwa gazeti hili wiki hii mjini hapa kuhusu kukamilika kwa rasimu ya kwanza ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2013.


“Ni kweli Sera hiyo imekamilika baada ya kuandaliwa kwa miaka mitatu. Imepita kwa wadau mbalimbali, mashuleni, vyuoni na katika taasisi mbalimbali nchini ambao wametoa maoni yao. “Jumapili (kesho) tunatarajia kuwa waheshimiwa wabunge nao watapata fursa ya kuijadili na kutoa maoni yao katika semina iliyoandaliwa maalumu kwao,” alisema Mulugo katika Viwanja vya Bunge.

Alisema baada ya maoni hao ya wabunge, watapeleka Rasimu hiyo kwa mamlaka husika kwa ajili ya andiko la mwisho kabla ya kupelekwa katika Bunge lijalo ili itungwe sheria kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo.

Hata hivyo, semina hiyo huenda isifanyike kesho kutokana na kuingiliana na ratiba nyingine, kwani wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakuwa na mkutano na Mwenyekiti wao wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kwenye Ukumbi wa White House mjini hapa.


Wiki moja iliyopita, wakati akiongoza kikao, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwaambia wabunge kuwa makabrasha waliyokuwa wakipewa na wahudumu ni kuhusu Sera ya Elimu na hivyo waende wakayasome, kwani kuna siku wataijadili.

Kwa mujibu wa rasimu, mambo mengine yanayotarajiwa kutekelezwa na Sera ni kuhuisha mitaala ya sasa ya elimu ili ikidhi muundo mpya wa elimu na mafunzo, kuhuisha sheria na taratibu mbalimbali za utoaji elimu ili ziendane na muundo mpya wa elimu-msingi.


Kuimarisha mfumo wa usimamizi, ithibati na udhibiti wa utoaji wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali ili kukidhi malengo na muundo mpya wa elimu-msingi.

Nyingine ni kuongeza ubora wa miundombinu katika shule za sasa za msingi ili kukidhi mahitaji na malengo ya elimu-msingi ikiwa ni pamoja na kuongeza madarasa ya elimu-msingi katika kila shule ya msingi ya sasa, kujenga maabara za sayansi na maktaba katika kila shule ya elimu-msingi.


“Kutenga rasilimali fedha za kutosha kwa ajili ya nyenzo, vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia, vitabu vya kiada na ziada, maandiko, machapisho ya maktaba pamoja na vifaa vya maabara,” ilieleza rasimi hiyo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza katika ngazi ya elimu – msingi kama lugha za kujifunzia na kuwasiliana.


Kuweka utaratibu utakaohakikisha kuwa wanafunzi wanaomaliza elimu na mafunzo ngazi husika kwa ufanisi na wale wanaokatisha masomo au mafunzo yao kwa sababu mbalimbali, wanaendelea na kuhitimu masomo au mafunzo yao katika mfumo rasmi wa elimu na mafunzo. Jambo jingine litakalotekelezwa ni kutoa elimu kwa umma kuhusu madhumuni, malengo na matarajio ya Sera mpya ya Elimu na Mafunzo.

Rasimu ilieleza kuwa mambo chanya yanayotarajiwa kupatikana baada ya mkakati kutekelezwa ni kuwepo kwa elimu ya awali ya lazima kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja kabla ya kujiunga na elimu msingi, kuwepo kwa elimu msingi ya miaka 10 kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne cha sasa kwa watoto wote wenye rika la kwenda shule.


Matokeo mengine ni kuwepo kwa mfumo nyumbufu, miundo na taratibu za kujiendeleza katika mikondo anuai ya kitaalamu na kitaaluma, kuwepo kwa elimu na mafunzo yenye viwango, ubora na sifa zinazotambulika kitaifa, kikanda na kimataifa.


“Kuwepo kwa fursa mbalimbali za elimu na mafunzo zinazokidhi mahitaji ya wananchi na ya nchi kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia.


“Kuwepo kwa ugharimiaji endelevu wa elimu na mafunzo na kuwepo kwa mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatia masuala mtambuka,” ilifafanua Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo.


Kuhusu elimu ya awali, ilieleza kuwa mkakati ni kuweka vigezo, viwango na taratibu ili elimu ya awali iwe ya lazima na itolewe katika kila shule ya elimu – msingi, na kuwa sheria, miongozo na taratibu kuhusu elimu hiyo lazima kuwekwa na kutekelezwa ifikapo mwaka 2018.


Katika elimu msingi, ni kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, na kutolewa kwa miaka 10 na umri wa kuanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.

Shabaha katika eneo hili ni sheria na miongozo kuhusu elimu-msingi kuwekwa na kutekelezwa ifikapo mwaka 2016, mpango wa utekelezaji wa utoaji wa elimu-msingi kuwepo ifikapo mwaka 2018 na elimu-msingi kutolewa ifikapo 2018.


Kwa mujibu wa dibaji ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Sera mpya imeandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau ikitilia maanani mafanikio yaliyoletwa na Sera zilizotangulia na kulifanya Taifa kupiga hatua katika nyanja za elimu na mafunzo.
 
“Sera kuu zilikuwa ni Sera ya Elimu na Mafunzo 1995, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo 1996 na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu 1999 ambazo zilitekelewa sambamba na sera nyingine ambazo zinaigusa sekta ya elimu na mafunzo kama vile Sera ya Sayansi na Teknolojia 1996, Sera ya Habari na Utangazaji 2003, Sera ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na ya Binafsi 2009 pamoja na nyingine za aina hiyo,” alisema Dk Kawambwa.