Showing posts with label KIJAMII. Show all posts
Showing posts with label KIJAMII. Show all posts

Wednesday, November 4, 2015


Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeahirisha kwa mara ya pili  hafla ya vyama vya siasa kumuaga Rais Jakaya Kikwete baada ya  kumaliza miaka 10 ya uongozi wake kwa mujibu wa katiba. 
 
Hafla hiyo inayoratibiwa na Baraza la Vyama vya Siasa ilipangwa  kufanyika jana baada ya Oktoba 2, mwaka huu kuahirishwa ili kutoa  fursa kwa Rais Kikwete kushughulikia mvutano wa uchaguzi wa Zanzibar  ulioibuka kufuatia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kufuta matokeo  yote ya uchaguzi huo. 
 
Vyama vilivyoalikwa kushiriki hafla hiyo ya kumuaga Rais Kikwete ni  Chama Cha Mapinduzi (CCM), vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya  Wananchi ( Ukawa) vya Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf), NLD na vyama  vingine vya upinzani.
 
Akitangaza kuahirishwa kwa hafla hiyo  kwa mara ya pili, jijini Dar  es Salaam jana, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi,  alisema kikao hicho kimeahirishwa tena kutokana na Rais kubanwa  na  majukumu mengine ya kitaifa ikiwamo suala la Zanzibar.
 
 “Tumeamua kuahirisha  hadi siku tutakayotangaza tena kutokana na  Rais kukabiliwa na majukumu mengine na suala la Zanzibar bado  linashughulikiwa,” alisema.
 
Alisema akiwa msajili wa vyama vya siasa  amefurahishwa na hatua ya  Rais Kikwete  kulishughulikia suala la Zanzibar  kwa vitendo ili   kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa  nchini.

Friday, September 4, 2015


Mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa Awamu ya Tano, ataunda tume tatu ikiwamo ya kuchunguza upya sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili ambalo utekelezaji wake ulilalamikiwa na wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda mkoani hapa, Lowassa alitaja tume nyingine kuwa ni za kuchunguza mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa la Efatha na wananchi na mgogoro kati ya wakulima.

“Kuhusu Operesheni Tokomeza wananchi wengi wamekuwa wakija kuniona na kunieleza wazi kuwa licha ya madhara yaliyojitokeza katika operesheni hiyo hawakulipwa, pia walipoteza haki zao, ndugu na mifugo."

Lowassa aliyetokea Namanyere alikofanya mkutano mwingine wa kampeni, aliwataka wananchi kuichagua Ukawa, kwa maelezo kuwa umoja huo utaleta mabadiliko.

Operesheni Tokomeza Ujangili ilibuniwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kupambana na ujangili ambao ulikithiri hadi taasisi za kimataifa kuingilia kati.

Hata hivyo, ilisitishwa Novemba Mosi, 2013 ili kupisha uchunguzi wa malalamiko yaliyojitokeza, yakiwamo ya wananchi kuuawa, kuteswa na kuporwa mali zao. 
 
Uchunguzi huo ulifanywa na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na sakata hilo lilipowasilishwa bungeni na kamati hiyo, lilisababisha mawaziri wanne kushinikizwa na Bunge kujiuzulu, kutokana na kuhusishwa na yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo.

Mawaziri waliong’oka ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Hamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Dk Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).

Hata hivyo, hivi karibuni Ikulu iliwaondolea doa mawaziri hao kutokana na ripoti ya Tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo kwa maelezo kuwa waliwajibika kisiasa na hawakuhusika moja kwa moja na vitendo hivyo na hakuna hatua inayostahili kuchukuliwa dhidi yao.
 
 Kuhusu mgogoro wa kanisa la Efatha na wananchi alisema: “Suala hili linalalamikiwa sana na kwa muda mrefu linawatesa wakulima na wawekezaji. Katika kuwalinda wakulima wadogowadogo itaundwa tume ili kuchunguza suala hili ili hatua za haraka zichukuliwe.”

“Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi kati ya wakulima na wafugaji, hasa waliopo katika Bonde la Mto Rukwa. Nitaunda tume ili kuhakikisha kuwa naondoa migogoro hii ambayo imedumu kwa muda mrefu,” alisema.

“Serikali yangu itanunua mahindi kwa wakulima na itawalipa riba. Haya ndiyo mabadiliko ninayoyataka. Wanaosema hawana sera wanajidanganya sana nawaambieni mkinipa kura nikaingia Ikulu wataisoma namba,” alisema.

Mbowe: Tumeunganisha nguvu
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Tumeunganisha nguvu za Watanzania wenye dhamira na mapenzi mema wanaotaka kuona mabadiliko ya nchi yetu. Tumempokea Lowassa kwa sababu tunaamini atatusaidia safari yetu ya kuwakomboa Watanzania.

“ Mgombea (Lowassa) ameteswa sana CCM na ndoto yake ya uongozi ilikuwa siku nyingi, lakini CCM hawakuiona hiyo na wakampuuza kwa maneno ya uongo.”

Mbowe alisema Rais Kikwete alimtosa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa urais na kushangazwa na kitendo cha Pinda kuendelea kubaki CCM.

Mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Lowassa nao walichukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM, lakini baada ya kutopitishwa kuwania urais walihamia Ukawa.

Kada mpya wa Chadema, Hamis Mgeja alisema: “Miradi ambayo Magufuli (Dk John) alishindwa kuijenga kwa ubora itajengwa na kumalizwa chini ya utawala wa Lowassa.

Monday, October 14, 2013


  
 ITV journalist Ufoo Saro is wheeled out of the operating room at Muhimbili National Hospital yesterday.  Ms Saro was shot and seriously wounded by her fiance, who also shot the reporter’s mother dead before taking his own life.  
PHOTO | EMMANUEL HERMAN

Dar es Salaam. 
The family of Antel Mushi was not aware he was in the country until he shot dead his fiancee’s mother before taking his own life on Sunday, according to a close relative.

Mushi, who was working with the UN in Sudan, also shot and seriously wounded Ms Ufoo Saro at her home in Kibamba, Dar es Salaam.

His elder brother, Mr Silver Mushi, said yesterday that a friend called him on the fateful day at around 9am, and asked him whether Antel had come home from Sudan after he heard on the radio and television that he (Antel) had shot and killed Ms Anastazia Saro, 58, and seriously wounded his fiancee, who is a reporter with ITV, before turning the gun on himself.

Mr Mushi said he last spoke to Antel on October 9, this year, when the latter was travelling on official duty within Sudan.

“He told me to pray for him...we did not speak again until I was called by a friend who alerted me about the radio and television reports,” he said.

Mr Mushi said Antel, 40, was a down-to-earth person “who had more friends than enemies”.

He added that he could not have even remotely imagined that his younger brother could do what he did on Sunday.

Mr Moshi said he last saw Antel in July when he came to Tanzania on leave, and recalled that Ms Saro saw her fiance off at Kilimanjaro International when he left for Sudan.

Antel received primary education in Moshi before he went to Zanzibar for his secondary education. He joined ITV in 1994 before joining the then Arusha-based International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR).

He left ICTR and joined the UN in Sudan where he was working as a telecommunications officer.

“He liked studying a lot and was at the time of his death undertaking distance learning through a university in India, and was due to graduate in December,” Mr Mushi said.
Antel lived with Ms Saro for about 13 years and the couple had a child

MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kufanya kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe. Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.

Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.

Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii Kocha’, Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.

Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.


 
                    Waumini wa dini ya kiisilamu wakipinga matumizi ya jina Allah kwa kikristo

Mahakama nchini Malaysia, imeamua kuwa watu wasio waisilamu wasitumie jina 'Allah' kumaanisha Mungu katika katika imani zao na kubatilisha uamuzi wa mahakama ndogo uliotolewa mwaka 2009.
Mahakama ya rufaa ilisema kuwa jina Allah linapaswa tu kutumiwa na waumini wa kiisilamu la sivyo linaweza kuzua taharuki miongoni mwa jamii.
Watu wa imani zote nchini Malaysia wanatumia neno Allah kumaanisha Mungu.
Wakristo wanateta kuwa wamekuwa wakitumia jina hilo la Allah katika lugha ya Malay na ambalo lilitokana na lugha ya kiarabu kumaanisha Mungu kwa miaka mingi na kuwa uamuzi wa mahakama unakiuka haki zao.
Mwanamke mmoja mkristo alisema kuwa uamuzi huo utaathiri jamii pakubwa.
"ikiwa tutawazuia watu wengine kutumia jila la Allah, basi itatubidi kutafsiri Bibilia nzima upya" Ester Moiji kutoka jimbo la Sabah aliambia BBC.
Umauzi ulitolewa na mahakama ndogo mwaka 2009 ulisababisha taharuki baina ya waisilamu na wakristo huku makanisa na misikiti ikishambuliwa.
Ilitokea baada ya serikali kusema kuwa jarida la kikatoliki la The Herald, haliwezi kutumia jina Allah katika makala yake ya lugha ya Malay kumaanisha Mungu kwa kikristo.
Wahariri wa jarida hilo lilikwenda mahakani kupinga uamuzi huo na mahakama ikafanya uamuzi uliowapendelea. Serikali baadaye ilikata rufaa.
Lakini katika uamuzi wake leo, jaji alisema kuwa jina Allah haliwezi kutumika kwa dini ya kikrsito kumaanisha Mungu na kuwa ikiwa jina hilo litatumiwa basi huenda likazusha taharuki baina ya jamii.
Mhariri wa jarida hilo alisema kuwa alighadhabishwa na kushangazwa sana na uamuzi wa mahakama na kwamba atakata rufaa.
Wafuasi wa jarida hilo wamesema kuwa Bibilia zilizoandikwa kwa lugha ya Malay zimekuwa zikimtaja Allah kumaanisha Mungu kwa kikristo tangu zamani sana.





....KWELI DUNIA WAWILI WAWILI.....

HUYU KIJANA AISHI KWA TABU KUTOKANA NA WATU WAMUONAPO HUANZA KUKIMBIA HUKU WENGINE WAKIMZONGA KUTOKANA NA KUFANANA SANA NA MAREHEMU STEVEN KANUMBA.

Sunday, October 13, 2013



Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere [1922-1999]

HAYA NI MAMBO 11 ALIYOYAPINGA BABA WA TAIFA-MWL. NYERERE


Ni miaka kumi na tatu sasa imepita tangu mzee wetu mpendwa baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aiage dunia.

Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 13, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria . Alikuwa ni mototo wa chifu Burito Nyerere wa kabila dogo la wazanaki

Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi [kwa saa za Afrika Mashariki], katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.

Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani. Mwalimu bado ni taa inayong’aa gizani, umuhimu wake nazidi kuonekana kadiri miaka inavyokwenda licha ya kwanza amekwisha tuacha.

Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere alichukia na kukemea vikali mambo yasiyofaa kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania , Afrika na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya mambo hayo ni:

1. UJINGA
Mwalimu Nyerere alikuwa ni miongoni mwa wasomi wachache na ni mtanzania wa kwanza kupata nafasi yamasomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Edinburg , Uingereza na kuhitimu mwaka 1952 akiwa ni gwiji wa uchumi na historia.

Mwalimu hakupenda ujinga na hivyo alipigana vita kali dhidi ya ujinga, na alifanikiwa kwa nafasi yake kuwaondoa ujinga watanzania wengi, wakiwemo viongozi wetu wa sasa ambao walisomeshwa ‘bure’ katika mazingira mazuri yakuridhisha kwa manufaa ya nchi yetu. Ndiyo maana Rais Kikwete Februari 3, 2007 alisema “….sisi tuliwekezwa na ni lazima tuwekeze kwenu ili miaka 30 ijayo Rais atoke miongoni mwenu….”

Kama Nyerere asingechukia ujinga kwa kuboresha mazingira ya elimu, ikiwemo elimu ya watu wazima, basi leo hii tungekuwa na vingozi ‘zezeta’.

Vita ya ujinga sasa si yakuridhisha. Zaidi ya asilimia 28.6 ya watanzania hasa waishio vijijini hawajui kusoma na kuandika, pamoja na kutoa elimu ya msingi bure na kupunguzwa ada ya sekondari na kuongeza idadi ya madarasa, bado shule hizi zinakosa waalimu na vifaa vya kutosha. Pia idadi kubwa ya watanzania pamoja na kufaulu hawapati nafasi ya elimu ya juu kutokana na sera chakavu na mifumo kndamizi iliyopo nchini, kama ya kuangalia madaraja [Division] katika utoaji wa mikopo na asilimia za uchangiaji gharama za elimu ya juu.

Kuna usemi usemao “If education is Expensive try ignorance as your option” [kama elimu ni ghali, jaribu ujinga]. Serikali yetu ni wazi kabisa kuwa inaona elimu ni gharama, hivyo imeamua kujaribu ‘ujinga’ kwa kile inachokiita ‘kuchangia elimu ya juu’ eti serikali haina uwezo.

Huku ndiko kuzienzi kuzienzi fikra za Mwalimu Nyerere?

2. UBINAFSI NA UFISADI
Katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo wa aina yake, ni pamoja na masuala ya haki na usawa. Mwalimu siku zote, alijenga imani katika misngi ya utu, haki na usawa kwa kila raia wa dunia hii. Aidha Mwalimu alipinga sana mianya ya unyonyaji aliyoiita ‘mirija’. Mwalimu alipinga sera zozote zinazweza kuleta matabaka katika Taifa, iwe ni matabaka ya kiuchumi kwa kuwa na kundi la walionacho na wasionacho. Mwalimu hakuruhusu ubinafsi na ufisadi ambao ambao leo hii umekithiri miongoni mwa viongozi wengi hapa nchini. Mwalimu aliwahi kusema “Hakuna mtu yeyote katika jamii atakayekuwa na mahitaji yote muhimu wakati wengine katika jamii hiyohiyo hawana chochote”.

Mwalimu alijikita katika siasa ya ‘ujamaa’ na kujitegemea na hatimaye Azimio la Arusha mwaka 1967, ili kahakisha keti ya Taifa [National cake] inakuwa na mgawanyo sawa kwa wote.Leo hii Azimio la Arusha limesahauika kabisa, hali ya viongozi wa serikali wanatanguza mbele maslahi binafsi hali ambayo baba wa Taifa aliipinga tabia hiyo chafu inayozidi kuchukua sura mpya kila kukicha.

Mwaka 1978 nchi yetu ilikuwa katika wakati mgumu wa vita dhidi ya Nduli Iddiamin Dada, lakini wabunge walihitaji nyongeza ya mishahara na kupunguzwa posho ya waanafunzi wa elimu ya juu. Hali hii ilipelekea wanafunzi wa enzi hiyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kugoma na kupinga ubinafsi wa waung hao. Hapa tuliona msimamo, uzalendo na busara za Mwalimu aliyetoa kauli kali ya kuamuru mishahara ya wabunge ipunguzwe na posho za vijana zibaki kama awali.

Nyerere asingekuwa mzalendo wa kwelil basi leo hii familia yake wangekuwa ndio mabilionea wan chi hii.

3. UBEPARI
Mwalimu alikuwa ni nuru ing’aayo gizani, alipinga mfumo wa ubepari kwa kuuita ‘mfumo wa ufukarishaji’. Hivyo aliimarisha misingi imara katika itikadi yake ya ujamaa na kujitegemea, ikiwa ndiyo itikadi pekee yenye misingi ya utu, haki na usawa.

Mwalimu alichukizwa sana na mfumo mpya wa kibepari uliozuka baada ya yeye kung’atuka madarakani aliouita ‘ubepari wa pembezoni’ yaani ni ubepari wa kishenzi unaotoa mianya kwa wachache kutumia mirija kuwanyonya wanyonge.

Tanzania yetu leo hii, bila hata aibu katiba ya Jamhuri ya Muungano katika ibara yake ya 3 inasema, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Hili linaleta utata na mkangnyiko kwani kimaandishi ni wajamaa lakini matendo yaliyopo ni zaidi ya ubepari.

Unaweza kuangalia uuzwaji holela wa nyumba za serikali zilizojengwa kwa jasho la Mzee Nyerere na akina Rashid Kawawa, pamoja na mikataba mibovu inayotanguliza maslahi ya wachache.Mwalimu hakusita kukemea mambo ya kihuni kama haya.

Katika kitabu chake Ungozi wetu na hatima ya Tanzania ukurasa wa 28 Mwalimu alisema “Halimashauri kuu ya Taifa iliketi unguja, ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi, na walikuwa na haki ya kufanya hivyo maana sera ni yao.Ubaya wao ni kwamba, jambo lenyewe walilifanya kwa hila na janjajanja na mpaka sasa wanaendelea kuwadanganya wananchi kwamba sera ya CCM ni ya ujamaa na Kujitegemea.”

4. UKABILA NA USEHEMU
Wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam , alifanikiwa kuwaunganisha wanafunzi katika jumuiya moja iitwayo USARF ikijumuisha wanafunzi kutoka nchi zote za Afrika. Aliona kuwa ni vema kwani Afrrika ni moja. Leo hii wanafunzi wetu wanajitambulisha na kujitanabaisha kwa makabila na sehemu watokazo. USARF imekufa kabisa na imebezwa na vijikundi vya makabila yao . Hali hii ya ukabila na usehemu inatawala kona zote za nchi yetu na ndiyo maana watu wengi wakienda kuomba kazi au hata huduma katika sehemu fulani, utasikia anaulizwa ‘wewe ni kabila gani au unatoka mkoa gani?’Hapa tulipofikia nchi yetu imepotea kisiasa, kijamii na hata kiuchumi.

Naamini Roho ya Mwalimu Nyerere inahuzuika sana kuona wanafunzi wanavyomkumbuka wakidai haki zao hasa katika vipindi vya migomo, wakati hili ambalo aliasisi hawalienzi.

5. UBINAFSISHAJI HOLELA WA MALI ZA UMMA
Wakati wa uhai wake Mwalimu alilaani vikali ubinafsishaji holela wa masirika ya umma. Alwakataa Mabeberu waliojiita ‘wawekezaji’ walionuiya kufirisi utajiri wan chi yetu huku wakishibisha matumbo yao .

Leo hii vigogo wa serikali wanajichukulia majumba ya serikali bila kujali wao kutoka madarakani watumishi wa umma hapo baadaye wataishi wapi.

Huku ndiko kumuenzi Mwalimu, aliyekataa kuishi kwenye nyumba kubwa kule Butihama, akisema yeye sio tembo? Uko wapi uzalendo aliotuachia Mzee Nyerere?

6. KUONGOZWA KWA RIMOTI NA NCHI MATAJIRI
Nakumbuka siku moja Mwalimu Nyerere akiwa katika viwanja vya mnazi mmoja [ Dar es salaam ] aliwahi kusema “Tangu lini IMF ikawa International Ministry of Finance?” [Wizara ya fedha ya kimataifa].

Leo hii viwanja hivyohivyo vinatumika kuusifu ubeberu wa IMF na wawekezaji wake, huku tukiwekewa masharti magumu ya kuongoza nchi yetu kwa maslahi ya mabeberu.

Mwalimu aliwaonya mataifa tajiri wasiingilie mambo yetu ya ndani, pale walipoona maslahi yao hayazingatiwi, mara kwa mara walimuhoji Mwalimu ambapo yeye aliwaamuru waondoke haraka na misaada yao yote. Mwalimu hakupenda misaada ya kinafiki iliyolenga kuwaangamiza wananchi wake, alipinga amri na maagizo ya taasisi za fedha kama Benki ya Dunia [WB] na IMF [International Monetary Fund].Hivyo aliheshimu maamuzi yake sahihi katika kulinda heshima ya nchi yetu na watu wake.

Kipindi chote cha uhai wake Mwalimu alisisitiza haja ya mataifa ya Afrika kujitawala na kuwa huru katika kujiamulia mambo yake.

“Inapotokea taifa kuuza uhuru wake kwa ajili ya misaada ya kiuchumi au kukubali kukaliwa na majeshi ya nje, taifa hilo linakuwa limepotea na litanyonywa na watu wake watakuwa wanakandimizwa popote pale” alisema Mwalimu.

Kama tungekuwa na misimamo kama Nyerere, tungeheshimika. Lakini leo hii Mwalimu angefufuka angefadhaika sana kuona jinsi tunavyomuenzi.

7. UBABE NA VITISHO KATIKA UONGOZI

Mwalimu aliamini kuwa kiongozi bora hapaswi kuwa na jazba na asiyetumia ubabe wala vitisho katika maamuzi au katika kutatua tatizo ambalo jamii inataka litatuliwe kwa maslahi na manufaa ya Taifa. Aliamini kuwa kiongozi bora ni yule anayeruhusu mianya ya majadiliano baina yake na wale anaowaongoza. Asiyetumia lugha chafu au kashfa na kejeli kwa watu wake.

Leo hii tawala mbalimbali zikiwemo taasisi za elimu ya juu na hata chombo cha juu kabisa cha maamuzi [Bunge] vinatumia ubabe na vitisho katika maamuzi.

Tunashuhudia migomo ya vyuo vikuu kila kukicha huku maamuzi ya ‘kibabe’ yakitumika na watawala wa vyuo katika kukandamiza haki za wanafunzi. Masikini wanafunzi hawa wanabaki wanalia huku wakiimba “… kama siyo juhudi zako Nyerere na ...angesoma wapi…”

Tunaona pia Bunge linavyopitisha maamuzi yasiyo na maslahi kwa wananchi ‘kibabe’ na hata kuadhibu wale wanaojaribu kutetea maslahi ya wanyonge. Bunge hilohilo linatumia pia lugha za kejeli na dharau kuwatisha wananchi, ubabe na vitisho si misingi ya demokrasia na utawala bora.

8. UMANGIMEZA NA UKIRITIMBA

Wakati wa uhai wake Mwalimu aliheshimu mipaka, taasisi za utawala na mali za umma. Alichukia matumizi mabaya ya rasilimali za umma, pia aliheshimu mawazo yake mwenyewe na ya wenzake.

Mwalimu aliamini kwamba, kiongozi asiyepeda ukiritimba na umangimeza ni lazima awe mfuasi mzuri wa maadili anayoyasimamia, mwaminifu na mwadilifu kwa manufaa ya Taifa lake. Mwalimu hakupenda kutetea uovu wa viogozi eti kwa kutunza heshima zao au kulinda vyama vyao bila kujali uhusiano wao wala majina yao .

Hivyo katika serikali yake Mwalimu hakuawa na ubia na mtu yeyote duniani.

Leo hii ni viongozi wangapi wanadumisha fikra na misimamo ya Mwalimu kwa vitendo?

9. USIRI WA MIKATABA NA MAKAMPUNI YA KIGENI

Mwalimu alisisitiza uwazi katika mikataba mbalimbali ambayo serikali iliingia na makampuni ya kigeni.

Katika kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo Mwalimu anasema “Viongozi wa kiserikali wana wajibu mkubwa wa kuwafahamisha wananchi nini serikali inafanya na kwa sababu gain”

Tofauti kabisa hali ilivyo sasa, hali inayopelekea minung’uniko na malumbano yanayo husisha hata ugawaji wa tenda za serikali. Labda tuangalie mfano mmoja tu wa Mkataba wa Buzwagi ambao ulikuwa ni maarufu kama ‘Mkataba wa Karamagi’ kati ya Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi na Kampuni ya Barrik Gold Mine.

Mkataba huu ulikuwa ni siri kubwa baina ya Barrik na Waziri tu, hali iliyopelekea Mbunge Zitto Kabwe kusimamishwa shughuli za bunge kwa miezi minne baada ya yeye kuhoji uhalali na uharaka wa utiaji saini mkataba huo uliosainiwa hotelini [Churchil Hotel] mjini London Uingereza.

Hivi nchi yetu itakuwa kituko mpaka lini? Mbona hatuoni viongozi wanaoleta tija na maendeleo.

Nakumbuka Rais Thabo Mbeki wa Afika Kusini alitudharau sana alipokuwa katika moja ya ziara zake hapa nchini, alisema wakati biashara ya Tanzanite inatoa dola milioni 500 kwa mwaka duniani, Tanzania nchi pekee duniani yenye madini hayo inapata dola 80 tu.

Rais Mbeki alitukejeli kwa kusema hakuna sababu ya kumtafutamchawi wakati sheria ya uchimbaji madini tumeitunga wenyewe inayoruhusu wageni waondoke na asilimia kubwa ya madini hayo na sisi kuambulia mashimo.

Hali hii inanipa shaka hasa nikichunguza upeo wa kufikiri wa hawa viongozi wetu, ndipo ninapokumbuka usemi wa Waziri mstaafu Arcado Mtagazwa [CCM] alioutoa bungeni mwaka 1993, alisema “Tutakapokufa vizazi vijavyo vitafukua makaburi yetu ili vione vichwa vyetu viongozi vilikuwa na ubongo wa aina gain kwa sababu yaelekea hatufikiri sawasawa”.

Kauli hii ililazimika kutolewa baada ya kuona kwamba baadhi ya maamuzi yanayofikiwa na serikali yetu hayana maslahi kwa taifa na ni ubinafsi.

10. RUSHWA
Katiba ya CCM katika ahadi yake ya nne [4] ina sema “rushwa ni adui wa haki, sitatoa rushwa wala kupokea rushwa”. Jambo la rushwa pia Mzee wetu mpendwa Mwl Nyerere alilikemea vikali enzi za uhai wake kwani alijua wazi kuwa rushwa ni kikwazo cha maendeleo ya umma katika kila Taifa.

Leo hi inchi yetu imegubikwa na rushwa na hata kuhalalishwa na kuitwa ‘takrima’ ili tu kukidhi matakwa na mahitaji ya ‘mahafidhina’. Viongozi wa serikali, viongozi katika taasisi mbalimbali wameweka mbele rushwa kama msingi wa kushibisha matumbo yao. Baya zaidi hata viongozi wa CCM chama pekee kilicho asisiwa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere wamezisahau kabisa falsafa zake na chuki yake dhidi ya rushwa na hata katika Chaguzi mbalimbali za Chama Cha mapinduzi zilizofanyika siku chache zilizopita tumeweza kusikia kama sio kushuhudia vitendo vya rushwa vikifanyika waziwazi katika chaguzi hizo jambo ambalo licha ya kushindwa kutumia mamlaka aliyonayo katika kuviasaidia vyombo husika kuchukua hatua za kisheria amebaki akilalamika na kushtaki kwa wananchi kuhusiana na vitendo hivyo vichafu vinavyotendeka ndani ya CCM, Serikali na hata katika sekta nyinginezo nyingi nchini.

Nakumbuka Mh Kabuye [Mb-TLP] aliwahi kuwashutumu bungeni kuwa anauhakika wabunge wote waliingia kwa rushwa, wabunge hao walioshutumiwa walimtaka Kabuye afute kauli naye alisema “ kwa kulazimishwa nafuta kauli”. Walimlazimisha lakini hoja yake ilibaki kuwa ni ya msingi.

11. UCHU WA MADARAKA
Mwl Nyerere ni miongoni mwa viongozi wachache sana duniani waliokosa kuwa na uchu wa madaraka. Ni miaka 24 sasa tangu Mwl ang’atuke madarakani kwa hiari yake akiwa kama rais wa awamu ya kwanza wa nchi yetu na ni miaka 22 tangu aachie uongozi wa CCM kama Mwenyekiti wa chama. Ndipo alipoamua kwa hiari yake kurejea Butihama na kuendeleza kilimo.

Uroho wa madaraka leo hii umekithiri, viongozi wengi wanaendelea kung’ang’ania madaraka bila kujali uzee walionao. Mahafidhina hawa wamezoea kusema ‘vijana ni taifa la kesho’ ili wao wazee waendelee kuhujumu mali za nchi yetu. Na unafiki wao ni pale wanaposema ‘vijana ni nguvu kazi ya taifa’, sentensi hizi mbili kimantiki zinakinzana. Mbaya zaidi na kinachouma ni pale unapoona watoto wa vigogo au viongozi wa Serikali wakiwa ndio kama warithi wa nafasi za wazazi wao ndani ya CCM na hata Serikali ya CCM.

Hili linaweza kujithibitisha wazi iwapo utaamua kufuatilia kwa undani idadi ya watoto wa vigogo na Viongozi waliomo ndani ya CCM sambamba na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi [CCM]



Alfajiri  ya  leo, mtangazaji  wa  ITV   anayejulikana  kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.
Akizungumza na Jungu Kuu,  kamanda Wambura  ambaye  ni kamanda  wa polisi wa  mkoa wa kipolisi wa kinondoni  amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
 
Kamanda wambura amedai  kuwa mwanaume  aliyetenda  mauaji  hayo ni  mchumba  wake  na  alikuwa anafanya  kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.

Kwa  mujibu  wa  Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili  awasuluhishe
Baada  ya  usuluhishi  kuanza  na  kuonekana  kuwa  tatizo  liko  kwa  mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa  na  mazoea  ya  kumtetea mwanae   na  ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo....
Alipomuua  mama  huyo, mwanaume huyo  alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.


Saturday, October 12, 2013

 
Msanii wa Filam Tanzania ajulikanae kwa jina la Wolper yuko hoi Hospitalini huku akiomba Dua kwa wapenzi wake wamuombee ili apone haraka. Wolper ameripot taarifa za kuumwa kwake katika akaunti yake ya facebook na kuainisha ugonjwa unaomsumbua ni Maralia na ujumbe huo umesomeka hivi: clip_image002


NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima. Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.


AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.

MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha.
MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake, wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli ya kazi za ndani.
Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano iliyopita.


Friday, October 11, 2013

 

Tarehe 20/09/2013 majira ya saa 4 mpaka saa 5 usiku Huko Buhongwa mtaa wa Ihila wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza yalitokea mauaji ya watu watatu wa familia moja ambao ni James Elias (44), Lucia James (35) pamoja na mtoto wao aitwaye Eliudi James umri wa mwaka mmoja.

Mauji hayo yanasadikika kufanywa na Lameck Paul (33) mkazi wa igombe wilayani Ilemela jijini Mwanza aliyekuwa mgeni katika familia hiyo kuanzia tarehe 17/09/2013 ambaye alitoweka mara baada ya kufanya tukio hilo.

Muuaji huyo alifika nyumbani kwa marehemu tarehe 17/09/2013 ili kufanya kibarua cha kufyatua matofali kwaajili ya ujenzi wa Nyumba ya matofali na walitegemea kuianza tarehe 22/09/2013  kwa muda wa siku nne.

Muuaji huyo alielewana na marehemu James Elias kwamba ameuza kiwanja chake huko maeneo ya Buswelu na pesa hiyo alitaka kuitumia kujenga nyumba ya pili na ndio maana alimtafuta kwaajili ya kumfyatulia matofali  ili  apate  pesa.

Muuaji alimshawishi marehemu ampe kiasi chochote cha pesa kama malipo ya awali kwenda kulipa huko Igombe alikokuwa akidaiwa fedha ambayo ilikuwa ni fidia ya mifuko miwili ya sementi aliyokuwa ameiba siku za nyuma.

Baada ya kugundua kuwa marehemu hakuwa tayari kutoa pesa aliyokuwa anahitaji, muuaji  huyo alijenga dhamira ya kumuua marehemu ili achukue pesa yote.

Majira ya saa 4 na saa 5 usiku Lameck Paul alitoka nje na aliporudi alikuwa tayari amechukua shoka na kuaanza kumshambulia kichwani kwa kumkatakata kichwani na sehemu ya chini ya sikio la kushoto hali iliyosababisha mauti.

 Baada ya kumuua alimuita mke wa marehemu aliyekuwa amelala chumbani na alipotokeza alimshambulia kwa shoka na kuangukia chumbani, alimfuata na kumnyonga  kwa waya wa umeme.

Mauaji yaliendelea baada ya mtoto mdogo wa mwaka mmoja aliyekuwa amelala na mama yake kuanza kulia ndipo muuaji alimchukua na kumnyonga kwa kutomia waya ule ule aliomnyongea mama yake.

Polisi waliendelea kumsaka mtuhumiwa huyo na mnamo tarehe 5/10/2013 mtuhumiwa alikamatwa akiwa nyumbani kwa mganga wa kienyeji Anastazia Joseph (38), mkazi wa kijiji cha Hinduki - Malampaka wilayani Maswa ambapo alikuwa akifanyiwa zindiko ili asikamatwe.

Mtuhumiwa alikiri kufanya mauaji hayo na kuiba kiasi cha pesa Tsh. 200,000/= suruali mbili na T-shirt moja, radio ndogo nyeusi, simu mbili za mkononi aina ya Nokia na  mashine ya mahesabu (Calculator).

Mtuhumiwa alirejeshwa mkoani Mwanza kwa ajili ya kuonyesha shoka alilotumia kufanyia mauaji.

 Mnamo tarehe 7/10/2013 majira ya saa za mchana katika maeneoya mtaa wa Ihila kata ya Buhongwa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza askari wakiwa na mtuhumiwa huyo wakielekea eneo alikoficha shoka alilotumia kufanya mauaji, baada ya kufika eneo la tukio kundi la wananchi waliitokea  maeneo mbalimbali wakiwa na mawe na fimbo na kuanza kuwashambulia askari na mtuhumiwa wakiwa na lengo la kumuua mtuhumiwa ambapo walimshambulia na kusababisha kifo chake.

Baadhi ya askari wamejeruhiwa, Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa Bugando kwa uchunguzi zaidi.

Taarifa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.




Sunday, July 21, 2013






<

Wednesday, June 5, 2013


Msafara wa kupokea mwili wa msanii  marehemu Albert Mangwea ukiwa unaingia morogoro hapa ni eneo la nane nane,Umati mkubwa umejitokeza katika mapokezi hayo jioni ya leo

 
 MAPOKEZI YA MWILI WA NGWEA ENEO LA MAZIMBU ROAD KIHONDA.